Nenda kwa yaliyomo

Emin Pasha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eduard Schnitzer aliyejulikana kama Emin Pasha

Mehmet Emin Pasha (28 Machi 1840 - 23 Oktoba 1892) alikuwa daktari, mtaalamu na gavana wa jimbo la Equatoria la nchi ya Misri. Kwa asili alikuwa Mjerumani lakini alifanya kazi hasa katika Milki ya Osmani.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Emin Pasha alizaliwa kwa jina la Isaak Eduard Schnitzer mjini Opole (leo nchini Poland), wazazi wake wakiwa Wayahudi. Baada ya kifo cha baba mwaka wa 1845, mama aliolewa tena na kubatizwa pamoja na watoto wake kuwa Wakristo.

Alihitimu chuo kikuu cha Berlin katika somo la tiba mwaka wa 1864 na kuondoka moja kwa moja hadi mji wa Konstantinopoli ili kufanya kazi chini ya Milki ya Osmani.

Kuanzia mwaka wa 1875 alitumia jina la Mehmet Amin; wakati huo aliishi mjini Khartoum (nchini Sudani). Mwaka wa 1878 alimfuata Charles George Gordon kuwa gavana wa jimbo la Ekwatoria. Tangu mwaka wa 1881 alilazimishwa kujitegemea katika jimbo lake kwa sababu ya uasi wa Muhammad Ahmad.

Mwaka wa 1886 alipewa cheo cha Pasha. Mwaka wa 1888, Emin Pasha alikombolewa na Henry Morton Stanley, nao pamoja wakaanza safari ya kwenda Bagamoyo ambapo walifika mwaka wa 1890.

Emin Pasha aliuawa na Waarabu wawili wakati alipochunguza maziwa ya Afrika Mashariki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emin Pasha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.