Omar al-Bashir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
al-Bashir kwenye mkutano wa 12 wa Umoja wa Afrika mwaka 2009

Omar Hasan al-Bashir (amezaliwa 1 Januari 1944) ni Rais wa nchi ya Sudan.

Alikuwa rais tangu 1993. Alitangulia kushika mamlaka nchini baada ya kuwa kiongozi wa uasi wa kijeshi uliopindua serikali ya waziri mkuu Sadiq al-Mahdi mwaka 1989. Bashir aliongoza nchi kama mwenyekiti wa kamati ya wanajeshi na baadaye waziri mkuu hadi kujipa cheo cha rais 1993.

Baada ya kushika uongozi alishirikiana na mwanasiasa na kiongozi wa Kiislamu Hassan al-Turabi akatangaza sheria zilizoweka nchi chini ya muundo wa shari'a ya Kiislamu. Alikandamiza wapinzani vikali mwishowe pia mshauri wake wa awali al-Turabi.

Mwaka 2004 Bashir alikubali mkataba wa amani uliomaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Sudan Kusini akaipa sehemu hii ya nchi haki ya kujitawala. Lakini vita ya ndani nyingine ilianza katika Darfur (Sudan magharibi). Kutokana na mauaji mengi na matendo ya kinyama dhidi ya watu raia Al-Bashir ameshtakiwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya jinai kama mkosaji wa jinai dhidi ya binadamu.

Al-Bashir anaandaa kugombea urais tena katika uchaguzi wa kitaifa mwaka 2010 ambao ni uchaguzi wa kwanza baada ya miaka 10 unaotarajiwa kuwa na vyama vingi.

Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Omar al-Bashir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.