Mahakama ya Kimataifa ya Jinai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
Rais wa Sudan Omar al-Bashir ambaye anatakiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu katika eneo la Darfur

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (Kifaransa: Cour Pénale Internationale; Kiing. International Criminal Court ambayo kawaida hujulikana kama ICC au ICCt ni mahakama ya kudumu ya kuwashtaki watu kwa mauaji ya kimbari, hatia dhidi ya ubinadamu, hatia za kivita na hatia ya ushambulizi (ingawa kwa sasa haiwezi kuwashtaki watu kwa hatia ya ushambulizi). Makao makuu yako Den Haag (Uholanzi).

Ni tofauti na Mahakama Kuu ya Kimataifa inayoamua ugomvi kati ya nchi kama pande zote zinakubali kupeleka kesi huko.

Msingi wa ICC[hariri | hariri chanzo]

Mahakama haya yaliundwa mnamo tarehe Mosi Julai, mwaka wa 2000 - tarehe ambapo Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ulipata nguvu za kisheria.

Kufikia mwaka wa 2010, nchi 110 ni wanachama wa mahakama hayo, na nchi zingine 38 zimetia sahini lakini hazijapitisha kisheria Mkataba wa Roma. Hata hivyo, mataifa mengi, ikiwemo Uchina, Uhindi, Urusi na Marekani zinazidi kuyakosoa mahakama hayo na hazijajiunga nayo.

Kesi mbele yake[hariri | hariri chanzo]

Hadi 2011 mahakama imepokea malalamiko kuhusu kesi katika nchi 139; hadi Machi 2011 utafiti rasmi umefungulia kwa kesi 6, zote katika Afrika: Uganda Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Darfur (Sudan), Kenya na Libya. Kesi tatu zilipelekwa na nchi ambazo ni wanachama wa ICC (Uganda, Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati), mbili na Baraza la Usalama la UM (Darfur na Libya) na moja kufuatana na azimio la mshtaki mkuu wa ICC (Kenya).

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.