Nishati mbadala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nguvu ya upepo ni chanzo muhimu cha nishati mbadala

Nishati mbadala ni aina za nishati kutoka vyanzo asilia kama vile mwanga wa jua, nguvu ya upepo, mvua, joto kutoka ardhi, mwendo wa kupwakujaa, kuni au aina nyingine za biomasi na mengine.

Kwa jumla ni vyanzo vya nishati visivyokwisha kutokana na matumizi au kupoa haraka, tofauti na fueli za kisukuku ambazo zinatoka kwenye vyanzo kama makaa mawe, gesi asilia au mafuta ya petroli zinazoendelea kupungua kadiri zinazotumiwa.

Uwekezaji kwenye miradi ya nishati mbadala duniani ulifikia kiasi cha dola za Marekani bilioni 286 mwaka 2015, huku nchi za China na Marekani zikiongoza kwa uwekezaji.[1] Kazi zinazohusiana na nishati mbadala duniani zinakadiriwa kufikia milioni 7.7.[2] Nchi kama Iceland inatumia asilimia 85 ya mahitaji yake ya nishati kutoka nishati mbadala na hivyo kuwa nchi ya kwanza duniani kwa matumizi makubwa ya aina hii ya nishati.[3] Kutokana na ripoti iliyotolewa na REN21 (Renewable Energy Policy Network for the 21st Century', mwaka 2015 nishati mbadala ilichangia asilimia 19.2 ya matumizi ya nishati duniani.[4]

Matumizi ya nishati mbadala[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2008 takriban 19-20% ya matumizi ya nishati duniani yametokea kwenye nishati mbadala; sehemu kubwa ya takriban 13% kutoka biomasi hasa kuni na 3.2% kutoka nguvu ya umememaji. Vyanzo vipya kama umeme kutoka upepo, umeme wa nishatijua, joto kutoka ardhini na umeme kutoka mwendo wa kupwakujaa vilileta asilimia 3 pekee lakini kiwango hiki kinazidi kuongezeka haraka. [5]

Hali halisi manufaa kutoka nishati ya jua ni kubwa zaidi sana kwa sababu matumizi yote ya mimea, mazao na matunda yana nishati ya jua kama msingi wake; pia kiwango cha joto la mazingira kinasababishwa na jua lakini katika takwimu hizi zinataja viwango tu vinavotumiwa na jitihada za binadamu kubadilisha mazingira asilia kama kupasha moto nyumbani, kupika vyakula, uzalishaji umeme, kuendesha usafiri na kadhalika.

Katika uzalishaji wa umeme duniani asilimia ya nguvu ya umememaji ilikuwa takriban 15%.

Kuongezeka kwa nguvu ya upepo[hariri | hariri chanzo]

Teknolojia ya kuzalisha umeme wa upepo imepanuka sana katika miaka iliyopita. Mwisho wa mwaka 2009 ujazifu wa umeme kutoka chanzo hiki ulikuwa megawati 157,900 ambazo ni ongezeko la 31% tangu mwanzo wa mwaka uleule. [6]

Maendeleo hayo mwanzoni yalitokea Ulaya, hasa Ujerumani, Udani na Uingereza lakini baadaye Marekani na China ziliongeza pia jitihada zao kupanua chanzo hicho cha umeme. [7][8]

Katika nchi ya Denmark umeme kutoka nguvu ya upepo ni tayari asilimia 19 ya matumizi yote ya kitaifa. [9]

Umemenuru[hariri | hariri chanzo]

Nellis Solar Power Plant inazalisha umemenuru kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani.

Seli za umemenuru zinabadilisha mwanga wa jua kuwa umeme. Teknolojia hiyo inaendelea haraka sana na gharama za seli hizi zimeshuka. Kuna vituo vingi, hasa Ulaya, ambako serikali zimetoa misaada kwa ajili ya kutegeneza vituo hivyo na matumizi ya teknolojia hiyo. [10]

Mwisho wa mwaka 2010 vituo vikubwa duniani vilikuwa :

Vituo vikubwa zaidi hutengenezwa.[11]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nishati mbadala kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.