Joto kutoka ardhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mvuke unatoka kwenye kituo cha umeme wa joto kutoka ardhi ya Nesjavellir Geothermal Power Station nchini Iceland.

Joto kutoka ardhi, pia joto ardhi (Kiing. "geothermal energy" kutoka Kigiriki geo =ardhi na thermos = joto) ni chanzo cha nishati kinachotumia joto lililopo chini ya uso wa dunia.

Joto ndani ya dunia[hariri | hariri chanzo]

Kiini cha dunia ni ya moto sana kinafikia maelfu ya sentigredi[1]. Kwa jumla joto kubwa la ndani linapungua hadi uso wa dunia lakini kuna mahali ambako njia za magma (mwamba ya moto ulioyeyuka) zinafika karibu na uso wa dunia. Kama njia za magma zinafika usoni wa dunia moja kwa moja tunaona volkeno. Lakini mara nyingi zaidi kuna mahali ambako maji chini ya ardhi yanagusana na miamba ya moto iliyopo mita mamia chini ya ardhi.

Matumizi ya joto ndani ya ardhi[hariri | hariri chanzo]

Tangu siku za kale watu walijua mahali kadhaa ambako maji ya moto yanatoka kwenye ardhi kama chemchemi. Kama chemchemi hizi za moto zilikuwa karibu na makazi ya watu zilitumiwa kwa kuogelea au hata kupasha moto nyumba kwenye mazigira baridi.

Lakini siku za nyuma watu waligundua mbinu kulitumia joto kutoka ardhi kwa kuzalisha umeme.[2] Mwaka 2007 takriban gigawati 10 za umeme zilipatikana kutokana na matumizi ya jotoa kutoka ardhini ambazo zilikuwa 0.3% ya mahitaji yote ya umeme duniani lakini katika nchi kadhaa kama Iceland au Kenya asilimia ilikuwa kubwa zaidi.

Katika mazingira ya kivolkeno joto kutoka ganda linafikia uso wa dunia na hapa ni rahisi kutumia mvuke unaotoka au akiba za maji moto zilizopo mita chache chini ya uso wa ardhi kuendesha rafadha za kutengeneza umeme. Nafasi hii iko pia katika sehemu za Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki nchini Kenya ambako hadi sasa kuna vituo 3 vya joto ardhi katika Olkaria. [3].

Katika mazingira ya kawaida pasipo na volkeno au njia za magma zinazokaribia uso wa dunia kuna uwezekano kupeleka mabomba ardhini na kupitisha kiowevo kwa pampu katika mabomba haya chini ya ardhi. Tofauti ya joto kati ya kina ambako mabomba yanafikia na uso wa dunia hutumiwa kwa kupashaia nyumba joto au baridi.

Kama kiwango cha joto kinachotolewa ardhini hakizidi kiwango kinachozalishwa katika kina ya ardhi nishati inayopatikana hapa ni kama nishati mbadala.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Joto hili latokana na mchakato wa kinyuklia ndani ya tufe la dunia
  2. Earth Science. United States of America: Holt, Rinehart and Winston. 2001. uk. 211. ISBN 0-03-055667-8. 
  3. "Olkaria I Geothermal Power Plant". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-04-07. Iliwekwa mnamo 2011-05-14. 

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: