Gigawati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gigawati ni kizio cha nguvu kinacholingana na wati bilioni moja (wati 109).

Kizio hiki hutumika kutaja uwezo wa vituo vikubwa vya kuzalisha umeme au tabia ya mtandao wa umeme kieneo. Kwa mfano kituo kikubwa cha nyuklia nchini Ubelgiji huwa na uwezo wa kutoa gigawati 1.04. Ethiopia ina vituo vya umeme vinavyoweza kuzalisha gigawati 4.5[1].

Mahitaji ya Tanzania yamekadiriwa kuwa masaa ya gigawati 6.3 kwenye mwaka 2015, na 12-13 kwenye mwaka 2020[2].

Kwa upande wa matumizi, gigawati ni kizio kwa mahitaji ya nchi ndogo yenye mtandao mzuri wa umeme, au nchi kubwa ambako bado wananchi wengi hawana umeme kwenye nyumba, viwanda si vingi, au katika mikoa ya nchi ya viwandani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [www.oxfordenergy.org/wpcms/wp-content/uploads/2018/08/The-politics-of-renewable-energy-in-East-Africa-EL-29.pdf The Politics of Renewable Energy in East Africa], pdf kwenye tovuti ya Oxfordenergy.org, uk 3
  2. [www.ewura.go.tz/wp-content/uploads/2017/01/Power-System-Master-Plan-Dec.-2016.pdf Power System Master Plan Update 2016], United Republic of Tanzania, Ministry of Energy and Minerals, uk 11
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gigawati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.