Nenda kwa yaliyomo

Wati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wati (pia:watt) ni kizio cha kupimia nguvu. Kifupi chake ni W. Fomula yake ni kg·m2·s−3.

Inaelezwa kuwa ni nguvu inayotokea kama juli moja ya nishati inatumiwa kwa muda wa sekunde moja. Hivyo inawezekana kuiandika pia kama J/s.

Wati ni kizio cha vipimo sanifu vya kimataifa. Imepewa jina lake kwa heshima ya mwanafizikia na mhandisi James Watt (1736 - 1819).

Wati moja ni sawa na volti-ampea moja (1 V·A). Uwezo wa majenereta huonyeshwa kwa kutaja kiasi cha wati yanachoweza kuzalisha. Kwa majenereta makubwa, kama vile vituo vya umeme vya diseli, umememaji au nyuklia kiasi hutajwa kwa megawati.

Vizio vya wati Kifupi kwa namba
1 mW (femtowati) fW 0.0000000000000001 W 10−15 W
1 mW (picowati) pW 0.0000000000001 W 10−12 W
1 mW (nanowati) nW 0.0000000001 W 10−9 W
1 mW (mikrowati) µW 0.0000001 W 10−6 W
1 mW (miliwati) mW 0.001 W 10−3 W
1 mW (sentiwati) cw 0.01 W 10−3 W
1 mW (desiwati) dw 0.1 W 10−1 W
1 W (wati) W 1 W 1 W
1 W (dekawati) daW 10 W 101 W
1 kW (hektowati) hW 100 W 102 W
1 kW (kilowati) kW 1,000 W 103 W
1 MW (megawati) MW 1,000,000 W 106 W
1 GW (gigawati) GW 1,000,000,000 W 109 W
1 TW (terawati) TW 1,000,000,000,000 W 1012 W
1 TW (petawati) PW 1,000,000,000,000,000 W 1015 W

Vizio vidogo sana kama pW vinatumika katika makadirio ya redio na radar; vifaa vya kiganga kama EEG na ECG mara nyingi hupimwa kwa µW.

daW na hW hali halisi havitumiwi; kama balbu ina 60 W hatusemi "6 daW" wala "15 hW" kwa balbu ya 150 W.

Kilowati (kW) ni kizio kwa vifaa vingi vya kila siku, kwa mfano kwa matumizi ya jiko la umeme au pia nguvu ya injini. Injini ya gari la kawaida huwa na 30 kW hadi 80 kW.

Megawati (MW) ni kizio cha kupima injini kubwa sana kama injini za meli na manowari kubwa lakini vinginevyo hutumika kwa kutaja nguvu ya majenereta ya kituo cha umeme.

Vizio vikubwa zaidi vinaweza kutokea katika matumizi ya vifaa vichache kama laser kubwa ya majaribio au kutaja jumla ya uzalishaji wa nguvu wa lambo la majiumeme; kwa mfano lambo la magenge matatu huwa na nafasi ya uzalishaji wa 22 GW.

Terawati ni nguvu ya radi ya kawaida.

Petawati inaweza kutumiwa kutaja nishati ya jua: nishati yote inayofika kwa njia ya nuru yake duniani ni takriban 174 PW.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.