Nenda kwa yaliyomo

Balbu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Balbu yenye tako la skrubu
Balbu yenye tako la Kiingereza

Balbu (pia: globu; kutoka Kiing. light bulb au light globe) ni kifaa cha kutolea nuru ikiwashwa yaani wakati umeme unapitishwa ndani yake. Hutumiwa kama sehemu ya kifaa kikubwa zaidi kama taa ya umeme.

Balbu hufanya kazi yake kwa kipindi fulani tu baadaye inakwisha inahitaji kubadilishwa. Wakati wa kutoa nuru inashika joto na kwa balbu zenye uzi joto hii huwa na kiwango cha kumwumiza mtu anayeigusa. Ikibadilishwa ni lazima kuangalifu maana inawezekana kupigwa na umeme kama mtu anagusa soketi yaani upande wa taa inayoshika balbu.

Muundo ya balbu yenye waya

[hariri | hariri chanzo]

Balbu ya kutolea nuru iligunduliwa katika karne ya 19. Awali waya nyembamba ya platini iliwekwa ndani ya gimba la kioo lililoondolewa hewa yote; wakati umeme ulipitishwa kwenye waya hii ilipashwa joto hadi kutoa nuru. Balbu za kwanza hazikudumu muda mrefu kwa hadi Thomas Edison alifauli kuziboresha kwa kutumia nyaya za kaboni au aloi mbalimbali za metali na kujaza balbu kwa gesi kama arigoni au nitrojeni iliyozuia kuharibika haraka kwa nyaya za kung'aa. Tangu wakati wake taa za umeme zilianza kusambaa kote duniani zikabadilisha maisha ya watu kwa kuwapa uwezekano wa kuangaza nyumba na barabara wakati wowote kwa gharama ndogo.