Kituo cha umeme

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kituo cha umememaji huko Bavaria
Kituo cha umeme huko Taiwan

Kituo cha umeme ni kiwanda ambako umeme unatengenezwa. Kwa kawaida kina idadi ya majenereta yanayotumia teknolojia ya sumakuumeme. Mara nyingi nguvu ya kuzungusha jenereta inapatikana kwa kutumia mvuke wa maji yaani mwendo wa mvuka huzungusha rafadha inayoendesha jenerata.

Mvuke huu hutengenezwa kwa moja ya njia zifuatazo:

Vituo vingine vinatumia miendo asilia kama vile

  • Umememaji ambako nguvu ya mwendo wa maji kutoka mahali pa juu kutelemka chini inazungusha rafahda za jenereta
  • Kutumia nguvu ya upepo vilevile na vituo vyake vimeenea katika miaka ya nyuma kwa uzalishaji umeme

Injini ya mwako ndani inaweza pia kuendesha majenereta.

Katika miaka iliyopita vituo vikubwa vya umemejua vimejengwa na vimekuwa vyanzo muhimu vya umeme katika nchi mbalimbali.