Nenda kwa yaliyomo

Umemejua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Umemejua ni teknolojia inayobadilisha nishati ya nuru ya jua kuwa umeme. Umemejua ni matumizi ya pekee ya umemenuru yaani mchakato wa kutumia nguvu ya mnururisho wa sumakuumeme.

Umemejua ni njia mojawapo ya kutumia nishati ya jua; mbinu nyingine ni matumizi ya joto la Jua moja kwa moja, usanisinuru wa mimea na matumizi ya nguvu ya upepo ambayo ni pia umbo mbadala la nishati ya jua.

Kuongezeka kwa uwezo wa paneli za sola (solar photovoltaics) kwa kizio cha gigawati.

Umemejua huzalishwa kupitia seli za sola (solar cells). Seli hizo kimsingi ni matabaka mawili ya silisi au nusukipitishi nyingine yaliyounganishwa ilhali tabaka la chini lina kiwango cha boroni inayosababisha kutokea kwa chaji chanya na sehemu ya chini imepata kiwango cha fosferi inayosababisha chaji hasi. Kila seli huwa na viungo vya umeme vinavyowezesha kupita kwa mkondo unaofikia nguvu ya takriban nusu volti.

Seli nyingi huunganishwa kufanya paneli ya sola. Paneli za aina hizo zinaunganishwa mara nyingi kutosheleza mahitaji ya umeme ya majengo madogo na makubwa, vijiji au hata miji.

Kushuka kwa bei za paneli za sola kwa wati moja ya umeme.

Matumizi ya teknolojia ya umemejua yalipanuka haraka katika miaka iliyopita. Baada ya kutengenezwa kwa seli ya sola ya kwanza mnamo 1954 hadi miaka ya 1980 vifaa vyake vilikuwa ghali sana. Tangu kuongezeka kwa uzalishaji wake, bei zimezidi kushuka haraka. Leo hii umemejua unatosheleza asilimia 1 ya mahitaji yote ya umeme duniani, katika nchi kadhaa umeshakuwa chanzo muhimu cha uzalishaji wa nishati kwa wananchi na uchumi wa taifa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umemejua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.