Boroni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Boroni (Borium)
B-TableImage.svg
Jina la Elementi Boroni (Borium)
Alama B
Namba atomia 5
Uzani atomia 10,8 u
Valensi 2, 3
Kiwango cha kuyeyuka 2349 K (2076 °C)
Kiwango cha kuchemka 4200 K (3927 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0

Boroni ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 5 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 10.811. Alama yake ni B.

Tabia[hariri | hariri chanzo]

Boroni ni nusumetali au metaloidi ina valensi tatu. Elementi pekee yake haipatikani katika mazingira asilia duniani ila tu katika kampaundi kama vile borasi (Na2B4O7·10H2O ).

Umbo hobela au la fuwele[hariri | hariri chanzo]

Inapotapaswa kutoka kwa kampaundi zake hupatikana katika umbo hobela kama unga wa rangi kahawia au la fuwele nyeusi na ngumu isiyohami umeme. Boroni ni dutu ngumu duniani baada ya almasi na kati ya elementi zote ni imara dhidi ya nguvu ya mvuto.

Matumizi kiteknolojia[hariri | hariri chanzo]

Matumizi ya boroni ni katika teknolojia ya kihami na katika madawa ya kupausha au kung'arisha. Inatumiwa pia kama nyongeza katika aloy kwa ajili ya sehemu za eropleni zinazotakiwa imara ma nyepesi. Kwa teknolojia ya kinyuklia hutumiwa kama kinga dhidi ya nyutroni katika matanuri ya nyuklia.

Nafasi ya kibiolojia[hariri | hariri chanzo]

Kwa kiasi ndogondogo boroni ina kazi katika miili ya wanyama isipokuwa bado haijaeleweka ni kazi gani isipokuwa imeonekana ni muhimu.

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Boroni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.