Sisimizi
Sisimizi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Majimoto (Solenopsis sp.)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 19: |
Sisimizi ni familia ya wadudu wadogo wanaoishi katika jamii. Jamii hizi zinaweza kuwa na sisimizi makumi kadhaa tu au kuwa na mamilioni kulingana na spishi mbalimbali.
Makazi yao yapo mara nyingi chini ya ardhi au mahali pengine panapohifadhiwa kama chini ya jiwe kubwa au katika nafasi ndani ya miti. Wanatumia udongo na nyuzi za mimea kwa ujenzi.
Jenasi kadhaa kama vile siafu (Dorylus spp.) hawana makazi ya kudumu bali wanahamahama.
Mchwa hawako karibu na sisimizi hata kama wanafana nao katika mengi na kuitwa kwa Kiingereza "white ants" lakini wako katika nasaba nyingine pamoja na kombamwiko.
Majina ya aina za sisimizi kwa Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Chungu (aina inayouma)
- Nyenyerere (wadogo weusi)
- Majimoto (aina nyekundu inayouma vibaya sana)
- Samesame (aina nyekundu)
- Sangara (aina nyekundu)
- Siafu (jenasi Dorylus)
- Sungusungu (Megaponera analis)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Amblyoponinae (Apomyrma stygia)
-
Aneuretinae (Aneuretus simoni)
-
Dolichoderinae (Axinidris luhya)
-
Dorylinae (Siafu, Dorylus sp.)
-
Ectatomminae (Rhytidoponera metallica)
-
Formicinae (Sisimizi wafumaji, Oecophylla longinoda)
-
Heteroponerinae (Heteroponera mayri)
-
Leptanillinae (Leptanilla revelierii)
-
Martialinae (Martialis heureka)
-
Myrmeciinae (Nothomyrmecia macrops)
-
Myrmicinae (Crematogaster nigriceps)
-
Paraponerinae (Paraponera clavata)
-
Ponerinae (Sungusungu, Megaponera analis)
-
Proceratiinae (Probolomyrmex guineensis)
-
Pseudomyrmecinae (Tetraponera parops)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Macro photos - images of ants Ilihifadhiwa 9 Desemba 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sisimizi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |