Mdudu Mabawa-viwambo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Hymenoptera)
Mdudu mabawa-viwambo | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyuki-asali (Apis mellifera)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusuoda 2: |
Wadudu mabawa-viwambo ni wadudu wadogo sana hadi wakubwa kiasi wa oda Hymenoptera katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Jina ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanajulikana sana kama nyuki, nyigu, dondora na sisimizi k.m.
Takriban spishi zote zina mabawa kama viwambo, lakini spishi nyingine au wana wa spishi nyingine (kama sisimizi) hawana mabawa. Kwa kawaida majike wana mrija wa kutaga mayai unaoweza kuingiza mayai ndani ya kidusiwa au katika mahali palipo ngumu kufikia. Katika spishi nyingi mrija huo umetoholewa kuwa mwiba.
Spishi za nusuoda Apocrita zina kiuno chembamba sana lakini zile za Symphyta zina kiuno kipana.
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Arge taitaensis, Nyigu-msumeno
- Megaponera analis, Sungusungu
- Polistes fastidiosus, Dondora
- Sceliphron spirifex, Bunzi mweusi-na-njano
- Xylocopa caffra, Nyuki-bungu njano
Mwainisho
[hariri | hariri chanzo]- Nusuoda Symphyta
- Familia za juu:
- Nusuoda Apocrita
- Oda ya chini Aculeata
- Familia za juu:
- Apoidea (Nyuki, nyukibambi, nyigu-mchanga, bunzi n.k.)
- Chrysidoidea (Nyigu-kekeo n.k.)
- Formicoidea (Sisimizi)
- Vespoidea (Dondora, mavu n.k.)
- Oda ya chini Parasitica
- Familia za juu:
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Sungusungu
-
Mavu
-
Bunzi mweusi-na-njano
-
Dondora
-
Nyuki-bungu njano
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-viwambo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |