Nenda kwa yaliyomo

Siafu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siafu
Safu ya siafu
Safu ya siafu
Askari ya siafu
Askari ya siafu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropodi (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabavu angavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia ya juu: Formicoidea (Hymenoptera kama siafu)
Familia: Formicidae (Sisimizi)
Nusufamilia: Dorylinae
Jenasi: Dorylus
Fabricius, 1793
Nusujenasi: Anommus
Ngazi za chini

Spishi:

Siafu ni spishi za sisimizi za jenasi Dorylus katika familia Formicidae ya oda Hymenoptera, lakini kiutendaj, jina hilo hutumika kwa spishi zinazoshughulika juu ya ardhi, hasa za nusujenasi Anomma. Wakitafuta chakula au kuhama, huenda kwa safu ndefu kama jeshi, kwa hiyo mojawapo ya majina ya Kiingereza "army ants". Isipokuwa spishi chache huko [[Asia] wa kitropiki, wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Idadi ya spishi zinazotambulika hutofautiana kulingana na chanzo, lakini 60 inaonekana kuwa makadirio ya kuridhisha [1], ambazo 9 zimo katika Anomma. Nyingi za spishi za Dorylus zinabishaniwa kwa sababu maelezo yao yalitokana na tabaka moja tu la kijamii. AntWiki [2] inategemeza spishi 15 katika Kenya. Idadi sawa ya spishi zinajulikana kutoka Tanzania na Uganda, nyingi zikitokea katika nchi mbili au tatu. Walakini, spishi 3 tu za siafu wa kweli zimekubaliwa katika Afrika ya Mashariki nzima.

Spishi za sisimizi wenye tabia kama hiyo zimeainishwa katika jenasi ya Kiafrika Aenictus na idadi ya jenasi za Kiamerika. Spishi za Aenictus ni ndogo kuliko siafu nyingine na zina rangi ya kahawia iliyofifia hadi kukolea. Makoloni yao ni madogo kuliko yale ya Dorylus na huwinda sisimizi wengine hasa.

Kama sisimizi wote husaidiana katika kazi mbalimbali kama vile ulinzi, usafi, kutafuta chakula na kazi nyingine.[3]

Siafu hutambuana kwa kugusana vichwa kama ilivyo jamii ya sisimizi wote.

Spishi za Afrika ya Mashariki (siafu wa kweli)

[hariri | hariri chanzo]
  • Dorylus nigricans (Kenya, Tanzania, Uganda)
  • Dorylus stanleyi (Kenya)
  • Dorylus wilverthi (Kenya, Rwanda, Uganda)
  1. Orodha ya Sisimizi Duniani
  2. Ants of Kenya
  3. National Geographic (2011-05-10). "Ants". National Geographic | Animals. Iliwekwa mnamo 2019-06-17.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siafu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.