Wadudu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Insecta)
Wadudu
Maumbile ya mdudu: A. Kichwa, B. Toraksi (kidari), C. Fumbatio, 1. Kipapasio, 2. Mandibuli (taya), 3. Laboro (mdomo wa juu), 4. Palpi ya maxila, 5. Klipei, 6. Paji, 7. Verteksi (pia ya kichwa), 8. Pronoto, 9. Skutelo, 10. Elitra (mabawa ya mbele), 11. Pingili, 12. Spirakulo, 13. Mguu wa mbele, 14. Mguu wa kati, 15. Mguu wa nyuma.
Maumbile ya mdudu: A. Kichwa, B. Toraksi (kidari), C. Fumbatio, 1. Kipapasio, 2. Mandibuli (taya), 3. Laboro (mdomo wa juu), 4. Palpi ya maxila, 5. Klipei, 6. Paji, 7. Verteksi (pia ya kichwa), 8. Pronoto, 9. Skutelo, 10. Elitra (mabawa ya mbele), 11. Pingili, 12. Spirakulo, 13. Mguu wa mbele, 14. Mguu wa kati, 15. Mguu wa nyuma.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Nusungeli na oda:

Wadudu wa kweli (tazama mdudu) ni kundi la arithropodi wadogo kiasi ambalo lina spishi nyingi duniani. Kibiolojia wako katika ngeli ya Insecta.

Wadudu wanashirikiana kuwa na muundo wa mwili chenye pande tatu za kichwa mbele, kidari katikati na fumbatio nyuma, halafu jozi tatu za miguu na kwa kawaida jozi mbili za mabawa. Kwa nje kiwiliwili kinafunikwa kwa khitini yenye kazi ya kiunzi nje.

Hadi sasa wataalamu waliainisha zaidi ya spishi milioni 1 za wadudu na makadirio ni kwamba kuna spishi nyingi zaidi, labda hadi milioni 30.

Wadudu wanaishi takriban kila mahali duniani. Spishi nyingi zinapatikana katika sehemu za tropiki na idadi inapungua kwenye baridi. Lakini kuna hata spishi moja iliyopatikana Antaktika. Wadudu ni wachache sana baharini lakini hata humo kuna spishi chache.

Uainishaji[hariri | hariri chanzo]

Uainishaji wa wadudu umebadilika sana tangu utumiaji wa uchanganuzi wa ADN umeanza. Mfano wa mwainisho wa hivi karibuni unafuata:

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wadudu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.