Kiunzi nje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kichwa cha sisimizi: Chitini

Kiunzi nje ni ganda au ngozi imara inayobeba na kulinda mwili wa mnyama kwa nje si kwa ndani kama kiunzi cha mifupa.

Wadudu na arthropodi[hariri | hariri chanzo]

Ni hasa wanyama wa ngeli ya arthropodi kama vile wadudu, buibui na kaa wenye kiunzi nje imara ya chitini.

Kwa mnyama mdogo kiunzi hiki bado ni laini lakini kinaendelea kuwa kigumu. Baada ya muda kama mnyama anaendlea kukua ganda hili gumu linakuwa dogo. Hapo wanyama wenye kiunzi nje hutupa ganda na kukuza ngozi mpya itakayokuwa gumu tena.

Watu na kiunzi nje[hariri | hariri chanzo]

Watu wameanza kuiga mfumo wa wadudu kwa kujijengwa aina ya kiunzi nje.

Tangu kale wanajeshi waliwahi kuvaa suti za chuma au bapa mbalimbali za metali zilizokinga kifua, kichwa na tumbo.

Katika tiba kama mguu umevunjika unafunikwa bendeji ya plasta itakayokuwa mgumu; kwa muda ni ganda la nje linalobeba uzito wa mwili badala ya mfupa unaoendelea kupona.

Katika teknolojia ya kisasa muhandisi wanachunguza suti za kuvaa kwa wajeruhiwa au walemavu zitakazowezesha kutembea tena.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Biolojia[hariri | hariri chanzo]

Teknolojia[hariri | hariri chanzo]

Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiunzi nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.