Mdudu Mabawa-marefu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mdudu mabawa-marefu
Nzi-ning'inia wa Kimmins (Bittacus kimminsi) katika Afrika Kusini
Nzi-ning'inia wa Kimmins (Bittacus kimminsi) katika Afrika Kusini
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Mecoptera (Wadudu walio na mabawa marefu na miguu mirefu)
Hyatt & Arms, 1891
Ngazi za chini

Familia 9:

Wadudu mabawa-marefu ni wadudu wadogo wa oda Mecoptera (mèkos = urefu, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Familia muhimu za oda hii ni Panorpidae (nzi-nge) na Bittacidae (nzi-ning'inia).

Mabawa ya wadudu hawa ni membamba na marefu yenye vena nyingi zinazoikizika, kama yale ya wadudu siku-moja. Jenasi kadhaa zina mabawa madogo sana au zimepoteza mabawa kabisa.

Mwili vilevile ni mwembamba na mrefu. Fumbatio ya madume inafanana na mkia wa nge: imepindika juu na ncha yake ina umbo lililopapulika ambalo lina uchi wa kiume ndani yake.

Sehemu za kinywa za wadudu hawa ni sahili. Mandibuli ni ndefu zenye pedipalpi nene. Hukamata arithropodi wadogo au hula mizoga.

Lava wa wadudu mabawa-marefu wanafanana na viwavi wenye miguu sita mifupi ya kweli na miguu kadhaa ya bandia. Pingili ya kumi inabeba kisahani cha mfyonzo au jozi ya vikulabu. Hula maada ya mimea au wadudu waliokufa, pengine hukamata wadudu. Lava hugeuka kwa bundo katika udongo au ubao unaooza.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-marefu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hiyo kuhusu "Mdudu Mabawa-marefu" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.