Kiwavi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kipepeo na hali za kiwavi cha Schizura concinna.
Kiwavi cha hatua ya tano cha Opodiphthera eucalypti.

Kiwavi ni hatua ya ukuaji wa mdudu wa oda ya Lepidoptera (wadudu kama vipepeo na nondo). Kwa kawaida hula majani. Wakitokea kwa wingi, k.m. viwavijeshi, wanaweza kuharibu mimea na hasa mashamba. Hivyo ni adui wakubwa wa wakulima.

Jinsi ilivyo kwa wadudu wengi, maisha ya kiwavi huanza kama yai. Inatoka kwa umbo la kiwavi. Baada ya muda kiwavi huwa bundo. Ndani ya bundo hugeuka kuwa kipepeo anayetoka na kutaga mayai tena. Mzunguko huo kwa jumla ni metamofosisi.

Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiwavi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.