Nenda kwa yaliyomo

Mende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Blattodea)
Mende
Mende
Mende
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda
Ngeli: Insecta
Nusungeli: Pterygota
Oda ya juu: Dictyoptera
Oda: Blattodea
Von Wattenwyl, 1882
Ngazi za chini

Oda ya chini 1 ya mchwa; familia za juu 3 na familia 9 za mende:


Mende au kombamwiko ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda ya Blattodea (blatta = mende, eidos = umbo). Tangu mwanzo wa karne hii wataalamu wengi wamesadiki kwamba mchwa ni aina za mende wa kijamii[1][2]. Kwa hivyo oda yao, Isoptera, huwekwa ndani ya Blattodea kama oda ya chini mara nyingi. Kuna maainisho mengine pia[3]. Kundi la mchwa linajadiliwa katika ukurasa wake.

Kuna zaidi ya spishi 4,000 za mende, kati yao 30 hupatikana kwenye makazi ya watu, huku nne kati yao zinafahamika kama wadudu wasumbufu.

Miongoni mwa spishi zinazofahamika sana ni mende wa Amerika, ambaye ana urefu wa milimita 30, mende wa Ujerumani mwenye urefu wa milimita 15, na mende wa Asia anayekaribia urefu wa milimita 25. Mende wa kisasa ni wakubwa kidogo kuliko mende wa kale.

Mende-pori

Mende huishi katika mazingira mbalimbali ya duniani. Mende wasumbufu wanaweza kuishi maeneo mengi zaidi, lakini hupendelea maeneo yenye joto, kwa mfano ndani ya majengo. Mende wengi wa kitropiki hupendelea zaidi na joto na kwa hivyo katika kanda nje ya tropiki hushindwa kuishi nje ya majengo. Miiba iliyo miguuni kwa mende ilichukuliwa kuwa inaweza kuhisi lakini tafiti zimeonyesha ni mahususi kwa ajili ya kutembelea kwenye mchanga, nyavu na sehemu ambazo ni shida kutembea. Muundo wake wa miguu umechochea sana miundo kadhaa miguu ya mashine/roboti za binadamu.[4]

Mende huacha kemikali kwenye kinyesi chao, vile vile huacha harufu kwa ajili ya kujamiiana na kusongamana mende wengine watafuata njia / harufu hizi ili kufahamu chanzo cha chakula na maji pia kujua mende wengine wamejificha wapi.

Mende huchangamka zaidi usiku na hukimbia mwanga isipokuwa mende wa huko asia ambao wao hufuata mwanga.

Mende ni wadudu wakubwa spishi nyingi wana ukubwa wa dole gumba na baadhi huwa wakubwa zaidi mende mkubwa zaidi ni yule wa Australia, ambae alifikia urefu wa sentimita 9 na uzito wa gramu 30.

Mende wana miili bapa na kichwa kidogo, wanatabia nyingi kama wadudu, licha ya upekee mdogo na ni miongoni kati ya wadudu wa kale. Sehemu za midomo yao zipo chini ya kichwa na taya zao za kutafunia, wana macho makubwa mawili na antenna mbili kubwa na ndefu,

Jozi ya kwanza ya mbawa ni imara na ulinzi. Ambayo hulala kama kinga ya sehemu ya ndani na mbawa za ndani. Mbawa zote nnne zina matawi ya vena. Miguu yao ni migumu na yenye kucha tano kila mmoja. Fumbatio lake lina vipande kumi. [5]

Mayai na vipeto vyake

[hariri | hariri chanzo]
Mende jike, Blatella germanica, wenye kipeto (‘ootheca’) cha mayai.

Mende jike wakati fulani huonekana wakibeba vipeto vya mayai. Kipeto cha mayai cha mende wa Ujerumani hubeba mayai takribani 30 mpaka 40, membamba na yaliojipanga vema. Mayai hujiangua kutokana na mgandanizo wa hewa na kutoa tunutu ambao huendelea kupata hewa na huwa wengi na wagumu baada ya masaa manne kipindi cha mpito wakati wakuanguliwa na wakati wa kuvua. Magamba yaliozeeka ulizua hisia kwamba hao ndio mende zenuzenu kwanzia mende kukua mpaka kufikia umbo kamili huchukuwa miezi mine na kwaujumla mende huishi kwa muda wa mwaka mmoja tu. Mende jike anaweza kutaga mpaka mara nane katika maisha yake na kuzalisha mende takribani 300 hadi 400. Baadhi ya spishi mende hupewa mimba mara moja tu na kutaga mayai yake yote.

Kama wadudu wengine mende hujamiiana huku wadudu wengine wakiwa wanatizama pande tofauti, na tendo hili linaweza kuchukua saa kadhaa spishi nyingine huzaliana bila haja ya kuwa na dume.

Mende jike hupachika yai lake katika sehemu salama au hulibeba mpaka pale linapo karibia kuanguliwa. Baadhi ya spishi lakini huhifadhi mayai yao ndani ya miili yao au bila ya kipeto mpaka pale yatakayo anguliwa. Jenasi moja, Diploptera ni ya mtindo huu.

Tunutu wa mende kwa ukawaida ni sawa na mende wakubwa isipokuwa hukosa mbawa na viungo vya uzazi vinakuwa havijakomaa. Ukuaji waweza kuwa taratibu kufikia hata mwezi mmoja. Mende huweza hata kuishi kwa miaka minne.

Vipeto vya mende aina ya Periplaneta americana, Florianópolis, SC, Brazili.

Mende ni miongoni mwa wadudu walio wagumu duniani. Baadhi ya spishi huweza kudumu bila ya chakula kwa zaidi ya mwezi na wanaweza kuishi kwa kutegemea gundi kama ile ya kugundishia stempu tu.[6] Baadhi yao wanaweza kukaa bila ya hewa kwa dakika 45 kwenye baadhi ya jaribio mende walipona tu na na kuendelea kuishi baada ya kuzalishwa kwenye maji kwa muda wa dakika 30. [7]

Husemekana kuwa mende watabaki peke yao duniani kama binadamu wakijaribu kuiangamiza dunia kwa bomu la nyuklia kwani muda huweza kuhimili mionzi kwa zaidi ya mara 6 mpaka 15, kuliko binadamu wa kawaida.

Athari kama wadudu waharibifu

[hariri | hariri chanzo]

Mende naye ni miongoni mwa wadudu waharibifu kwenye makazi ya watu.hujilisha kwa chakula cha binadamu na mifugo na kuacha harufu mbaya sana. [8] Pia huweza kusafirisha vimelea vya magonjwa mpaka hata kwa binadamu hata mpaka vile vimelea ambavyo ni hatari kwa binadamu hasa katika mazingira hasa ya hospitalini.[9][10]

Namna bora ya kuangamiza mende ni kuweka vyakula vyote mbali kwenye vyombo vilivyo fugwa kutumia debe za taka zenye mifuniko imara, usafi wa mara kwa mara wa jiko na kuziba mabomba yatoayo maji.

Pia sehemu za nyumba zenye uwazi pia zizibwe kwa sababu mende huweza kuishi mpaka miezi mitatu bila ya chakula na maji hii hufanya vigumu wao kutoweka kabisa pindi wanapovamia makazi mapya.

Spishi kadhaa za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Mende

  1. Inward, D., Beccaloni, G. & Eggleton, P. 2007. Death of an order: a comprehensive molecular phylogenetic study confirms that termites are eusocial cockroaches. Biology Letters, 3(3): 331-335 [Published online 5 April 2007. doi: 10.1098/rsbl.2007.0102]
  2. "Termites are 'social cockroaches'", BBC News, 13 April 2007. 
  3. http://bugguide.net/node/view/601959/tree
  4. [1]
  5. [2]
  6. [3]
  7. [4]
  8. [5]
  9. [6]
  10. [7]