Mdudu Siku-moja
Mandhari
(Elekezwa kutoka Ephemeroptera)
Mdudu siku-moja | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu siku-moja (Ephemera danica)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nusuoda 3: |
Wadudu siku-moja ni wadudu wa oda Ephemeroptera (ephemeros = -a muda mfupi, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wadudu hawa huishi majini baridi katika muundo wa nayadi (lava ya wadudu wa maji) kwa muda wa mwaka mmoja, halafu hutoka kwenye maji na kuambua mara mbili na kuwa mdudu aliyekomaa wenye mabawa. Licha ya jina lao wadudu waliokomaa huishi muda wa nusu saa hadi siku kadhaa. Wanajamiiana tu na kutaga mayai; hawali na kwa hiyo wana alama za vipande vya mdomo tu na utumbo umejaa na hewa. Kinyume na wadudu waliokomaa nayadi hula viani na diatomea, na spishi kadhaa hula lava za wadudu wengine wa maji.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Furcatergalia – aliyekomaa (Leptophlebia marginata)
-
Furcatergalia – nayadi (Habrophlebia sp.)
-
Pisciformia – aliyekomaa (Baetis tricaudatus)
-
Pisciformia – nayadi (Cloeon dipterum)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Siku-moja kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |