Panzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Panzi
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis
Panzi kibyongo, Abisares viridipennis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Caelifera (Panzi)
Ngazi za chini

Oda za chini 2:

  • Acrididea
  • Tridactylidea

Panzi ni aina za wadudu wanaokula mimea. Waainishwa katika nusuoda Caelifera ya oda Orthoptera. Takriban spishi zote huchupa mbali kwa kutumia miguu yao ya nyuma ambayo ina nguvu sana. Nyingi zinaweza kuruka angani. Panzi wana vipapasio vifupi kuliko mwili wao. Panzi wakubwa ambao wanajikusanya kwenye makundi makubwa huitwa nzige. Kuna panzi wakubwa wengine wenye miiba mikubwa kwenye miguu ya nyuma lakini wasiojikusanya katika makundi. Panzi hao hufanana na ndege wadogo wakiruka juu na huitwa parare.

Panzi jike wana viungo vinavyowawezesha kuchimba ndani ya ardhi na kutaga mayai yao katika vibumba. Vibumba vya mayai huweza kuwa na mayai kumi na tano hadi zaidi ya mia moja. Mayai ya panzi aina nyingi huingia kwa diaposi kupitia majira ya baridi au kiangazi. Hali ya hewa ikiwa nzuri mayai yaendelea kupevuka halafu tunutu wanatoka. Tunutu (panzi wachanga) waambua ngozi zao mara tano mpaka mara saba kufuatana na aina yao. Kila hatua ya ukuaji ni kubwa kuliko ile iliyotangulia. Wakati wa uambuaji wa mwisho panzi mkubwa atokea na kuwa mpevu ndani ya siku au wiki chache.

Kuna wadudu ambao wanafanana na panzi lakini wana vipapasio virefu kuliko mwili wao. Aina moja kati yao anaitwa senene na huliwa na watu. Jike ana kiungo kama mfuo kinachofanana na kitara. Anataga mayai juu ya au ndani ya mimea.

Panzi huliwa sehemu nyingi duniani kwa sababu wana virutubisho (protini) vingi. Wanajeshi huambiwa wakamate panzi na kuwala wakipungukiwa chakula.

Mwainisho[hariri | hariri chanzo]

Kuna familia nyingi za panzi, lakini takriban spishi zote za Afrika ya Mashariki ni wanafamilia wa Acrididae na Pyrgomorphidae. Uainisho wa sikuhizi ni kama ufuatao (familia zote hazionyeshwi):

Familia na nusufamilia za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]