Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Panzi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nsenene

[hariri chanzo]

Mimi ni mkazi wa Mkoa wa Kagera ninaitwa Wilson Muhungye ninaishi Mji mdogo wa Kmachumu katika Wilaya ya Muleba,ninataka kujua chimbuko la wadudu "senene" wanatoka wapi au katika nchi gani mpaka kufika huku kwetu Bukoba?

Bwana Muhungye salaam. Asante kwa swali lako. Wana wa nsenene huishi porini ambapo hula wadudu wengine k.m. vidukari, nzi weupe na viwavi. Kwa hivyo wana hawa ni wadudu salihi. Nsenene wazima wanaweza kuwa waharibifu, kwa sababu hula mapunje ya mtama au mwele ambayo hayajaiva bado. Majira yakiwa mazuri, wana wengi wa nsenene hudiriki kuwa wazima na kujikusanya kwenye makundi makubwa yanayoweza kwenda makumi ya kilometa kwa siku. Usiku makundi haya huvutwa na mianga ya taa na hata ya moto. Mwishowe ninyi huwakamata ili kuwala. ChriKo (majadiliano) 14:55, 17 Mei 2012 (UTC)[jibu]