Nzige

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nzige
Nzige mwekundu, Nomadacris septemfasciata
Nzige mwekundu, Nomadacris septemfasciata
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Caelifera (Wadudu kama panzi)
Familia: Acrididae (Panzi)
Jenasi: Anacridium Uvarov, 1923

Calliptamus Serville, 1831
Chortoicetes Brunner von Wattenwyl, 1893
Dociostaurus Fieber, 1853
Locusta Linnaeus, 1758
Locustana Uvarov, 1921
Nomadacris Uvarov, 1923
Schistocerca Stål, 1873

Spishi: Angalia katiba

Nzige ni jamii ya panzi wenye uwezo wa kujikusanya kwenye makundi makubwa na kuruka umbali mrefu kwa pamoja. Wanao huitwa tunutu. Nzige wanapokuwa wametawanyika mmoja mmoja huishi kama panzi wa kawaida. Wanapozaliana na kuongezeka idadi hujikusanya katika makundi. Makundi ya tunutu husafiri kuelekea upande mmoja na kula majani wanakopitia. Makundi ya nzige waliokomaa huweza kufikia idadi zaidi ya bilioni na huruka umbali mrefu na kuharibu mazao wanakotua.

Udhibiti wa nzige[hariri | hariri chanzo]

Nzige hudhibitiwa kwa dawa za kikemikali. Afadhali nzige wadhibitiwe wanapokuwa wadogo au tunutu kabla wasiingie mashamba na kuharibu mazao. Tunutu wanaweza kudhibitiwa kwa mashine zinazobebwa mikononi au mgongoni, au zilizopachikwa juu ya gari la pickup. Makundi ya nzige waliokomaa lazima yadhibitiwe kwa ndege.

Hivi karibuni dawa ya kibiolojia imeendelezwa na mradi wa mataifa LUBILOSA. Dawa hii ina spora za kuvu Metarhizium acridum ndani yake. Siku hizi kuna vifundiro vya kibiashara vitatu sokoni: "Green Muscle" na "Green Guard" vya kampuni BASF na "NOVACRID" cha kampuni ÉLÉPHANT VERT. Vifundiro hivi vinaweza kupulizwa katika mafuta ya diseli kwa mashine za kiwango kidogo sana (g 50 katika L 0.5-2 kwa ha).

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Blue morpho butterfly.jpg Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nzige kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.