Spora

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Spora katika mzunguko wa maisha.

Spora ni jina la hatua ya uzazi bila ngono. Pengine huitwa kiiniyoga au kijimbegu pia, lakini jina la kwanza linafaa viyoga tu. Kwa kawaida spora zina seli moja tu na kuwa haploidi, yaani zina seti moja ya ADN. Viumbehai vyote vilivyo na seli zenye kiini, vina spora lakini zinaonekana vizuri tu katika protozoa, kuvu, miani na mimea ambayo sina mbegu (k.m. vigoga na aina za madege au majimbi).

Spora zinazoishi nje humea katika viumbe haploidi. Pengine viumbe hivi vinazaa spora tena, pengine vinamea kwa kuwa gametofiti. Kuna aina mbili za gametofiti: moja ina jinsia ya kiume na ingine jinsia ya kike. Kila aina inazaa gameti na lazima gameti moja ya kiume na moja ya kike ziungane ili kuwa zigoti. Halafu zigoti humea katika kiumbe diploidi, yaani kina seti mbili za ADN. Kiumbe hiki kitazaa spora tena.