Nenda kwa yaliyomo

Nzige

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nomadacris)
Nzige
Nzige mwekundu, Nomadacris septemfasciata
Nzige mwekundu, Nomadacris septemfasciata
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Caelifera (Wadudu kama panzi)
Familia: Acrididae (Panzi)
Ngazi za chini

Jenasi 12, spishi 16 za nzige:

Nzige ni jamii ya panzi wenye uwezo wa kujikusanya kwenye makundi makubwa na kuruka umbali mrefu kwa pamoja. Wanao huitwa tunutu. Nzige wanapokuwa wametawanyika mmojammoja huishi kama panzi wa kawaida. Wanapozaliana na kuongezeka idadi hujikusanya katika makundi. Makundi ya tunutu husafiri kuelekea upande mmoja na kula majani wanakopitia. Makundi ya nzige waliokomaa huweza kufikia idadi ya zaidi ya bilioni na huruka umbali mrefu na kuharibu mazao wanakotua.

Udhibiti wa nzige

[hariri | hariri chanzo]

Nzige hudhibitiwa kwa dawa za kikemikali. Ni vema nzige wadhibitiwe wanapokuwa wadogo au tunutu kabla hawajaingia mashamba na kuharibu mazao. Tunutu wanaweza kudhibitiwa kwa mashine zinazobebwa mikononi au mgongoni, au zilizopachikwa juu ya gari la pickup. Makundi ya nzige waliokomaa ni lazima yadhibitiwe kwa ndege.

Hivi karibuni dawa ya kibiolojia imeendelezwa na mradi wa kimataifa LUBILOSA. Dawa hiyo ina spora za kuvu Metarhizium acridum ndani yake. Siku hizi kuna vifundiro vya kibiashara vitatu sokoni: "Green Muscle" na "Green Guard" vya kampuni BASF na "NOVACRID" cha kampuni ÉLÉPHANT VERT. Vifundiro hivi vinaweza kupulizwa katika mafuta ya diseli kwa mashine za kiwango kidogo sana (g 50 katika L 0.5-2 kwa ha).

Katika Biblia

[hariri | hariri chanzo]

Nzige wanatajwa mara nyingi katika Biblia kati ya vitisho vikubwa kwa binadamu kutokana na njaa wanayoweza kusababisha.

Pia wanatajwa kama chakula maalumu cha Yohane Mbatizaji, mtangulizi wa Yesu.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nzige kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.