Mdudu mabawa-manyoya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mdudu mabawa-manyoya
Mdudu mabawa-manyoya (Hydropsyche pellucidula)
Mdudu mabawa-manyoya (Hydropsyche pellucidula)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Trichoptera (Wadudu wenye mabawa yanayobeba manyoya)
Kirby, 1813
Ngazi za chini

Nusuoda 2 na familia za juu 10:

Wadudu mabawa-manyoya ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Trichoptera (thrix = unyoya, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Jina lao ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanafanana na nondo wadogo (oda Lepidoptera) na oda hizi zina mnasaba. Lakini badala ya vigamba vya mabawa ya Lepidoptera mabawa ya Trichoptera yanabeba manyoya.

Lava wa spishi nyingi huishi majini lakini wale wa familia Limnephilidae huishi kwenye ardhi. Wanatoa hariri ili kuitengenezea utando au kipeto. Wanaotengeneza utando huishi katika maji yanayotiririka. Utando ni kimbilio na inafaa kutega chakula (wanyama wadogo, viani, masalio). Kipeto cha lava wengine (wadudu-kipeto) kinatumikia kwa kukinga kiwiliwili chororo dhidi ya adui na kinashirikisha vitu vigumu kama chembe za mchanga, vijiti, koa n.k. Lava anaweza kutoa kichwa na kidari (toraksi) na kutembea akivuta kipeto. Kuna lava ambao huishi majini bila utando au kipeto. Hawa hutumia hariri tu ili kutengeneza kifukofuko cha bundo.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Adicella vera
  • Anisocentropus fulvus
  • Athripsodes sagittatus
  • Cheumatopsyche meruana
  • Cheumatopsyche usambara
  • Chimarra elga
  • Chimarra kenyana
  • Chimarra somereni
  • Ecnomus dentatus
  • Ecnomus fuscus
  • Ecnomus mennelli
  • Helicopsyche annae
  • Helicopsyche bifida
  • Helicopsyche pedunculata
  • Helicopsyche stoltzei
  • Helicopsyche tanzanica
  • Helicopsyche usambarensis
  • Hydropsyche jeanneli
  • Hydropsyche plesia
  • Lepidostoma grana
  • Lepidostoma oma
  • Lepidostoma turka
  • Notoernodes inornatus
  • Oecetis caudata
  • Oecetis thikanensis
  • Pseudoxyethira glandulosa
  • Pseudoxyethira kenyella
  • Setodes gona
  • Setodes trifidus
  • Tinodes bicuspidalis
  • Tinodes guttatus
  • Tinodes rungweensis
  • Triaenodes elegantulus
  • Triaenodes hickini
  • Triaenodes tanzanicus
  • Ugandatrichia acuta
  • Ugandatrichia dentata
  • Ugandatrichia tanzaniensis

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu mabawa-manyoya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hiyo kuhusu "Mdudu mabawa-manyoya" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.