Nenda kwa yaliyomo

Mdudu Mikia-mitatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mdudu mikia-mitatu
“Kisamaki-fedha” (Lepisma saccharina)
“Kisamaki-fedha” (Lepisma saccharina)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Apterygota
Lang, 1888
Oda: Thysanura
Latreille, 1796
Ngazi za chini

Familia 5:

Wadudu mikia-mitatu ni arithropodi wadogo wa oda Thysanura (thysanos = nyoya yabisi, ura = mkia) katika nusungeli Apterygota (maana: bila mabawa) ya ngeli Insecta (wadudu wa kweli). Mikia mitatu ya wadudu hawa ni kwa kweli serki ndefu mbili na epiprokti iliyorefuka (“pingili” ya 11 ya fumbatio). Kiwiliwili chao ni bapa chenye umbo la yai au kimerefuka. Vipapasio ni kinamo na vipande vya mdomo ni vifupi na havikubobea. Hawana macho au macho ni madogo tu. Kiunzi-nje cha wadudu hawa si ngumu na kimefunikika kwa vigamba ambavyo vina rangi ya fedha mara nyingi. Kwa sababu ya hiyo na mwendo wao unaofanana na kuogelea, spishi kadhaa huitwa kisamaki-fedha. Kwa kawaida huonekana katika mazingira manyevu, pengine katika mazingira makavu. Visamaki-fedha huishi mara nyingi katika nyumba ambapo hula nafaka, lahamu, karatasi, wanga katika nguo, vitambaa vya rayoni na nyama iliyokauka. Spishi nyingine huishi katika mapango au katika vichuguu.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mikia-mitatu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hiyo kuhusu "Mdudu Mikia-mitatu" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.

Makala hii kuhusu "Mdudu Mikia-mitatu" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili silverfish kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni kisamaki-fedha.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.