Kichuguu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichuguu huko Chiuanga, upande wa Msumbiji wa ziwa Niasa.
Kichuguu tofauti.

Kichuguu (pia: kingulima, kiduta, kishirazi) ni sehemu au nyumba wanamoishi mchwa baada ya kujijengea kwa udongo waliouchanganya na mate yao.

Umbo linaweza kubadilika, lakini kuna masharti kadhaa ya kuwezesha mchwa kuishi (giza, ubichi n.k.).

Ili kichuguu kiwe hai lazima malkia awe hai kwani yeye ndiye anayetaga mayai kwa ajili ya kuzaa mchwa na kumbikumbi. Ndani ya kichuguu utakuta nyumba ya malkia ikiwa na ulinzi wa mchwa wengi sana.

Malkia huwa ni mweupe mwenye ngozi laini sana; kwa ndani ni kama ana majimaji au mafuta (kiowevu).

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kichuguu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.