Nenda kwa yaliyomo

Mbu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbu
Mbu wa aina ya anofelesi (Anopheles gambiae) akifyonza damu
Mbu wa aina ya anofelesi (Anopheles gambiae) akifyonza damu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Nematocera (Diptera wenye vipapasio kama nyuzi)
Latreille, 1825
Ngazi za chini

Oda za chini 7:

Mbu ni wadudu wadogo wa nusuoda Nematocera katika oda Diptera (yaani “wenye mabawa mawili”). Kwa asili jina hili limetumika kwa wadudu wa familia Culicidae, lakini kwa sababu spishi nyingi za Nematocera hazina majina ya Kiswahili, “mbu” linapendekezwa kama jina kwa Nematocera wote. Nusuoda nyingine ya Diptera, Brachycera, inashirikisha nzi na jamaa wao. Spishi ndogo za Nematocera huitwa usubi au visubi.

Diptera wote wana mabawa mawili tu yaliyopo kwa mesotoraksi. Mabawa ya nyuma ya asili yamepunguzika na kubadilika kuwa virungu (halteres) ambavyo vinasaidia mdudu ajue mkao wake na mabadiliko ya mwelekeo (kama aina ya gurudumu tuzi). Vipapasio vya Nematocera ni virefu kiasi na vina mapingili mengi kuliko Brachycera. Madume ya spishi nyingi zinabeba nywele nyingi juu ya vipapasio. Sehemu za kinywa za mbu zimetoholewa kwa kufyunza. Mara nyingi zinaweza kudunga, k.m. katika spishi zinazofyunza damu.

Spishi za mbu zinazojulikana sana ni zile ambazo hufyunza damu. Ni majike ambao wanafyunza damu, kwa sababu lazima wakuze mayai. Madume na spishi nyingine za mbu hufyunza mbochi au utomvu. Mbu waladamu hurithisha magonjwa mara nyingi, k.m. malaria (spishi za anofelesi (Anopheles)), homanyongo, homa ya vipindi, chikungunya (spishi za Aedes) na matende (spishi za kuleksi (Culex)).

Lava wa spishi nyingi zaidi huishi katika maji ambapo hula viani, bakteria na vijidudu wengine. Lava waambua ngozi mara nne kabla ya kuwa bundo. Akikomaa bundo aelea juu ya maji au apanda juu ya mmea wa maji na mdumili atoka.

Spishi kadhaa za Afrika

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.