Matende

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matende (Elephantiasis,
Lymphatic filariasis)
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10B74.
ICD-9125.0-125.9
eMedicinederm/888
MeSHD005368

Matende (kwa Kiingereza Elephantiasis, Lymphatic filariasis), ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa viungo vya mwili hasa miguu na viungo vya uzazi. Kuvimba huku kunasababishwa na mishipa ya limfu inayowaka na kutopitisha kiowevu cha limfu.

Ugonjwa unatokana na ambukizo la minyoo ya filaria unaoleta kuwaka kwa mishipa ya limfu.

Asili yake ni mara nyingi minyoo kimelea aina ya filaria. Mifano mingi ya maradhi hayo hayana dalili.[1] Angalau nyingine huvimba miguu, mikono au viungo vya uzazi.[1] Ngozi pia inaweza kuwa na unene na pengine kuumwa.[1]

Mabadiliko ya wazi ya mwili yanaweza kuleta unyanyapaa katika jamii na uchumi kwa mwathirika. [1]

Msamiati[hariri | hariri chanzo]

  • Elephantiasis = matende: inflamesheni ya kudumu, aghalabu ya miguu na jenitalia za nje inayoathiri ngozi na tishu sabukteni.
  • Matende = ugonjwa wa kuvimba miguu ambao huambukizwa na aina mojawapo ya mbu.
  • Filariasisi = ugonjwa utokanana na uambukizo wa minyoo ya filaria.
  • Lymphatics = mishipa ya limfu: mishipa ambayo husafirisha limfu.

Chanzo na uaguzi[hariri | hariri chanzo]

Minyoo wanasambazwa na umo wa mbu walioambukizwa.[1] Maambukizo kwa kawaida yanaanza kuwaumiza watu wakiwa bado watoto.[1]

Kuna aina tatu za minyoo wanaoambukiza maradhi hayo: Wuchereria bancrofti, Brugia malayi na Brugia timori.[1] Wucheria bancrofti inajulikana zaidi.[1] Minyoo wanaharibu (mfumo wa limfu)[1]

Maradhi huaguliwa kwa kutumia hadubini kwa kutazama damu iliyokusanywa usiku uliopita.[2] Lazima damu imeumbika katika mpako mnene na kutiliwa waa ya “Giemsa”.[2]

Kufanya jaribio kugundua fingomwili zizuiazo maradhi, pia kuna manufaa yake.[2]

Kinga na tiba[hariri | hariri chanzo]

Ugangakinga unafanikiwa kutokana na kutibu makundi ambamo maradhi yanaumia, kwa muda wa mwaka kukiwa na bidii yenye kutibu kabisa maradhi.[1]

Matibabu hayo kwa kawaida yanachukua muda wa miaka sita.[1]

Dawa zitumiwazo ni pamoja na “albendazole” pamoja na “ivermectin” au “albendazole” pamoja na “diethylcarbamazine”[1] Dawa hizo haziwaui minyoo wazima bali zinazuia kusambaa zaidi kwa maradhi hadi minyoo wenyewe wanapokufa. [1] Jitihada za kuzuia umo wa mbu zinapendekezwa zikiwa na jitihada za kupunguza idadi ya mbu pamoja na kuhimiza matumizi ya chandarua.[1]

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya watu walioambukizwa na matende inazidi milioni 120.[1] Takriban watu bilioni 1.4 wa nchi 73 wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa.[1] Maeneo ambayo yanaathirika zaidi yako katika Afrika na Asia.[1]

Maradhi hayo yanasababisha hasara ya kiuchumiː thamani yake ni mabilioni ya dola za Marekani kila mwaka.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 Lymphatic filariasis Fact sheet N°102. World Health Organization (March 2014). Iliwekwa mnamo 20 March 2014.
  2. 2.0 2.1 2.2 Parasites - Lymphatic Filariasis Diagnosis. CDC (June 14, 2013). Retrieved on 21 March 2014.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matende kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.