Nzi
Nzi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nzi-nyumbani (Musca domestica)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Oda za chini 6:
|
Nzi ni wadudu wadogo wa nusuoda Brachycera katika oda Diptera (yaani “wenye mabawa mawili”). Kwa asili jina hili limetumika kwa wadudu wa familia Muscidae, lakini kwa sababu spishi nyingi za Brachycera hazina majina ya Kiswahili, “nzi” linapendekezwa kama jina kwa Brachycera wote. Nusuoda nyingine ya Diptera, Nematocera, inashirikisha mbu na jamaa wao.
Diptera wote wana mabawa mawili tu yaliyopo kwa mesotoraksi. Mabawa ya nyuma ya asili yamepunguzika na kubadilika kuwa virungu (halteres) ambavyo vinasaidia mdudu ajue mkao wake na mabadiliko ya mwelekeo (kama aina ya gurudumu tuzi). Vipapasio vya Brachycera ni vifupi na vina mapingili machache kuliko Nematocera, mara nyingi matatu tu lakini hadi 7. Spishi nyingi zinabeba unywele (arista) juu ya pingili la tatu la vipapasio. Nzi hawana sehemu za kinywa zinazoweza kutumika kwa kutafuna, kwa hivyo hula chakula cha majimaji au cha chembe ndogo (kama chavua).
Lava wa nzi hawana miguu na wanafanana na minyoo. Kwa kawaida wana meno mawili yaliyopindika (kama kulabu) na spirakulo mbili kwenye nyuma ya kiwiliwili. Huonekana mara nyingi katika nyama iliyooza na katika matunda.
Spishi kadhaa za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Bactrocera dorsalis, Nzi wa Maembe (Mango fly)
- Calliphora vomitoria, Nzi Buluu (Blue bottle fly)
- Glossina swynnertoni, Mbung'o Masai (Swynnerton's tsetse)
- Musca domestica, Nzi-nyumbani (Housefly)
- Phaenicia sericata, Nzi Kijani (Common green bottle fly)
- Systoechus somali, Nzi-sufu Somali (Somali bee fly)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Asilomorpha/Asilidae (nzi mbuai Synolcus sp.)
-
Asilomorpha/Bombyliidae (nzi-sufu Systoechus gradatus: lava hula mayai ya panzi)
-
Muscomorpha/Muscidae (nzi-mazizi Stomoxys calcitrans)
-
Muscomorpha/Glossinidae (mbung'o-nyika Glossina morsitans)
-
Muscomorpha/Tephritidae (nzi wa maembe Bactrocera dorsalis)
-
Stratiomyomorpha/Stratiomyidae (nzi-jenerali Stratiomys chamaeleon)
-
Tabanomorpha/Tabanidae (pange Chrysops callidus)
-
Xylophagomorpha/Xylophagidae (nzi-mbao Xylophagus ater)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nzi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |