Mdudu Shingo-ngamia
Mandhari
Mdudu shingo-ngamia | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Raphidia ophiopsis
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia 6
|
Wadudu shingo-ngamia (kutoka kwa Kijerumani Kamelhalsfliegen) ni wadudu wakubwa kiasi wa oda Raphidioptera (raphio = sindano, ptera = mabawa) walio na shingo kama ngamia au kama nyoka (snakefly). Mabawa yao ni kama yale ya wadudu mabawa-vena, oda ambaye ndani yake wadudu hawa waliainishwa zamani. Wao ni wadudu mbuai na hula wadudu wengine wadogo, k.m. vidukari na matitiri. Hata lava hula wadudu wengine, mayai na lava hasa.
Wadudu hawa wanatokea katika misituni ya Nusudunia ya kaskazini. Kuna spishi tatu tu za wadudu shingo-ngamia katika Afrika kaskazini kwa Sahara. Hawatokei kusini kwa Sahara.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Africoraphidia spilonota
- Harraphidia harpyia
- Mauroraphidia maghrebina
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Raphidiidae (Ornatoraphidia flavilabris)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Shingo-ngamia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |