Utitiri (Arithropodi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Utitiri
Kifani cha utitiri mwekundu wa kuku
Kifani cha utitiri mwekundu wa kuku
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Nusungeli: Acari
Ngazi za chini

Oda za juu na oda:

Kwa asili jina utitiri hutumika kwa ugonjwa wa kuku ambao unasababishwa na wadudu wadogo walio na mnasaba na kupe na papasi. Lakini kwa sababu hakuna jina la jumla la Kiswahili kwa kundi la Acari “utitiri” hutumika zaidi na zaidi kwa spishi nyingine za Acari. Kwa asili pia neno hili lilikuwa nomino isiyoweza kuhesabiwa, kama sukari kwa mfano, lakini watu wengine wameanza kulichukulia kama neno katika umoja (pengine hata titiri) na "matitiri" kama wingi. Utitiri ni nusungeli katika ngeli ya Arachnida. Kwa hivyo wana miguu minane kama buibui na nge.

Utitiri ni arithropodi wadogo. Spishi kubwa kabisa zina mm 10-20, lakini takriban spishi zote ni ndogo au ndogo sana: spishi ndogo kabisa ina mm 0.05. Utitiri ni tele katika udongo ambapo husaidia kumeng'enya dutu ya viumbehai. Lakini spishi zinazojulikana zaidi ni vidusia vya nje vya wanyama na mimea. Mifano ya vidusia ni kupe, papasi, funduku na utitiri mwekundu.

Picha[hariri | hariri chanzo]