Nusutufe ya kaskazini
Mandhari
(Elekezwa kutoka Nusudunia ya kaskazini)
Nusutufe ya kaskazini (pia nusudunia ya kaskazini; Kiing.: Northern Hemisphere) ni nusu ya Dunia ilioko upande wa kaskazini ya ikweta.
Tofauti na nusutufe ya kusini hii kaskazini ya Dunia ina maeneo makubwa zaidi ya nchi kavu; theluthi mbili za nchi kavu za dunia ziko hapa kaskazini. Kwa hiyo pia sehemu kubwa ya binadamu hukaa kwenye nusutufe hii, ni asilimia 90 ya watu wote wanaoishi duniani.[1]
Kati ya mabara ni yote ya Ulaya, Asia na Amerika Kaskazini yaliyopo kwenye nusutufe hii.
Majira ya joto huwa ni hapa kuanzia Juni hadi Septemba, na majira baridi kuanzia Disemba hadi Machi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Nusutufe ya kusini
- Ikweta
- Tropiki ya Saratani
- Tropiki ya Kaprikoni
- Duara la Aktiki
- Duara la Antaktika
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Pretty Much Everyone Lives In The Northern Hemisphere , tovuti ya Business Insider ya May 4, 2012, iliangaliwa Agosti 2017