Mdudu-koleo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Dermaptera)
Mdudu-koleo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu-koleo (Anisolabis maritima)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nusuoda 4: |
Wadudu-koleo ni wadudu wadogo wa oda Dermaptera (derma = ngozi, ptera = mabawa) ambao wana serki kwa umbo wa koleo. Serki hizi hutumika kwa kushika mawindo, kwa kujitetea, kwa kukunja mabawa ya nyuma na wakati wa kujamiiana. Mabawa ya nyuma yakunjwa ili kufichwa chini ya yale ya mbele yaliyo mafupi.
Kuna spishi zinazoishi juu ya wanyama, lakini takriban spishi zote huishi nje na hula kila aina ya chakula: majani, maua, wadudu wadogo, maada ya mimea na wanyama waliokufa. Spishi kadhaa, kama mdudu-koleo wa Ulaya, zinaweza kuwa wasumbufu na kusababisha hasara katika mashamba. Lakini spishi nyingi zinasaidia wakulima kwa sababu wanakula wadudu wengine wasumbufu, kama vidukari.
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Anisolabis felix
- Anisolabis jeanneli
- Anisolabis maritima
- Dihybocercus confusus
- Isolabis bicolor
- Isolabis braueri
- Iolabis proxima
- Isolabis rufa
- Isolabis transversa
- Isolabis unicolor
- Isolabis usambarana
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Arixeniina: Arixenia esau (mdudu-koleo wenye manyoya)
-
Forficulina: Forficula auricularia (mdudu-koleo wa Ulaya)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu-koleo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |