Chungu (sisimizi)
Chungu | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mfanyakazi wa chungu (Camponotus cinctellus)
| ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||||
Spishi >1000; 36 katika Afrika ya Mashariki: |
Chungu spishi kubwa za sisimizi katika jenasi Camponotus ya nusufamilia Formicinae zinazotokea katika misitu ya mabara yote isipokuwa Antaktiki[1]. Kwa sababu hujenga makoloni yao ndani ya mbao, huitwa “carpenter ants” (sisimizi seremala) kwa Kiingereza. Ingawa spishi hizi sio kali sana, zinaweza kung'ata vinususi na kupuliza asidi fomi kwenye jeraha, ambayo huleta uchungu kali.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Chungu ni spishi kubwa za sisimizi ambao hujenga makao yao katika mbao nyevu zinazooza. Koloni lina malkia (wakati mwingine kadhaa), madume wapevu kadhaa na matabaka matatu ya wafanyakazi: wadogo, wa kati na wakubwa. Malkia wanaweza kuwa na urefu wa hadi sm 2.5, huku madume wakiwa na ukubwa takriban nusu[1]. Wafanyakazi wakubwa huwa wakubwa kuliko madume kwa kawaida. Wafanyakazi wadogo wanaweza kuwa wadogo kama sm 0.75 na wa kati wako kati bila shaka. Ingawa spishi nyingi na matabaka mengi ni nyeusi, zinaweza kuwa kahawia au mchanganyiko wa nyeusi, kijivu na kahawia. Spishi fulani hubeba nywele nyeupe, njano au kahawianyekundu.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Camponotus auropubens
- Camponotus braunsi
- Camponotus carbo
- Camponotus chrysurus
- Camponotus cinctellus
- Camponotus contraria
- Camponotus druryi
- Camponotus erinaceus
- Camponotus flavomarginatus
- Camponotus foraminosus
- Camponotus galla
- Camponotus heros
- Camponotus jeanneli
- Camponotus kersteni
- Camponotus kollbrunneri
- Camponotus limbiventris
- Camponotus maculatus
- Camponotus minusculus
- Camponotus mombassae
- Camponotus negus
- Camponotus niveosetosus
- Camponotus olivieri
- Camponotus orinobates
- Camponotus posticus
- Camponotus puberulus
- Camponotus pulvinatus
- Camponotus robecchii
- Camponotus rufoglaucus
- Camponotus sarmentus
- Camponotus schoutedeni
- Camponotus somalinus
- Camponotus troglodytes
- Camponotus vestitus
- Camponotus viri
- Camponotus vividus
- Camponotus zimmermanni
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Camponotus flavomarginatus
-
Kichiguu cha C. flavomarginatus
-
C. maculatus
-
C. niveosetosus
-
C. rufoglaucus
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Cranshaw, Whitney; Richard Redak (2013). Bugs Rule!: An Introduction to the World of Insects. Princeton Univ. Press. uk. 329. ISBN 978-1-4008-4892-8.