Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Umemejua

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tuchague jina lipi? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:59, 9 Machi 2019 (UTC)[jibu]

Nimejaribu kuangalia matumizi. Kwenye majarida nakuta mara nyingi umemejua (solar energy, solaelectric). Google inanipa kurasa 24.500 nikitafuta neno.
Umemenuru ina matokeo 277 pekee kwa google. Hali halisi kuna tofauti kati ya umemejua na umemenuru (photoelectric) yaani umemejua ni matumizi mojawapo wa umemenuru; naona watu wengi hawaoni tofauti hii maana ni jambo la elimu, nahisi haifundishwa katika elimu ya msingi hivyo wengi hawaelewi kwa Kiswahili.
Umeme-mwanga ni istilahi ninayokuta katika kamusi ya Kiingereza-Kiswahili ya TUKI for "photo-electric"; haiko katika kamui zote za Kiswahili-Kiingereza au Sw-sw. Hii labda pia wa sababu TUKI wanatumia zaidi "mwanga" pale ambako mimi nimetumia "nuru". (angalau Bakita wanapendelea "nuru", nisipokosei).
Napendekeza tuunde makala za umemenuru na umemejua. Unapenda kuanzisha? Kipala (majadiliano) 07:05, 9 Machi 2019 (UTC)[jibu]