Umemenuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Umemenuru (pia: umeme-mwanga, fotovoltaiki, kutoka Kiingereza photovoltaics, photoelectricity) ni umeme unaopatikana kutokana na nishati ya nuru hasa au kwa jumla kila aina ya mnururisho wa sumakuumeme. Badiliko hili linatokea katika seli zinazojulikana mara nyingi kama seli za sola. Seli ya umemenuru inatoa mkondo wa takriban nusu volti.

Nishati ya nuru ikikuta mata yenye tabia ya nusukipitishi (semikonda) inasababisha mwendo wa elektroni ndani yake. Nuru inaundwa na vipande vidogo vinavyoitwa fotoni. Nishati ya fotoni ikigonga elektroni inaweza kuiondoa katika nafasi yake kwenye mzingo elektroni na kusababisha kutokea kwa mkondo wa umeme.

Matumizi ya umemenuru yanapatikana katika teknolojia ya umemejua kwa uzalishaji wa umeme, lakini pia kwa vihisio (sensor) vya aina , mfano katika kamera au vifaa vya kupimia umbali, mwendo na kadhalika.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umemenuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.