Nenda kwa yaliyomo

Lambo la Magenge Matatu

Majiranukta: 30°49′23″N 111°00′12″E / 30.82306°N 111.00333°E / 30.82306; 111.00333
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lambo la magenge matatu)
Lambo la Magenge Matatu
Eneo la mto Yangtse na mahali pa mradi wa Magenge Matatu

Lambo la Magenge Matatu ni lambo kubwa nchini China katika eneo la magenge matatu ya mto Changjiang (Yangtse). Ni kati ya malambo makubwa kabisa duniani ikizalisha kiasi kikubwa cha nguvu ya umememaji kati ya malambo yote (22,250 megawati).

Shabaha ya lambo na eneo la mradi

[hariri | hariri chanzo]

Lambo lilikamilishwa mwaka 2008 kwa shabaha ya kuzuia mafuriko, kuzalisha umeme, kuendeleza uchukuzi, ufugaji samaki, utalii, kuhifadhi mazingira ya asili, kuboresha mazingira, kuhamisha wakazi katika maeneo ya ustawishaji, kupeleka maji kutoka sehemu ya kusini kwenda sehemu ya kaskazini na kumwagilia maji mashamba.

Sehemu ya juu ya ukingo wa maji ya bwawa ina urefu wa mita 3,035, maji baada ya kulimbikizwa katika hali ya kawaida ni yanakuwa na kina cha mita 175. Bwawa la maji la mradi huo linaweza kulimbikiza jumla ya mita za ujazo bilioni 39.3. Bwawa huwa na urefu wa kilomita 600 hadi mji wa Chongqing.

Mipango ya mradi

[hariri | hariri chanzo]

Mtu wa kwanza wa kuleta hoja la kujenga lambo hapa alikuwa Sun Yat-sen raisi wa kwanza wa China. Serikali za China na wakati wa vita pia Japan walifanya mipango ya ujenzi.

Katika miaka ya 1980 mradi ulianzishwa upya na kukubaliwa mwaka 1992 kwa kura katika bunge la China. Waziri mkuu Li Peng alikuwa mtetezi mkuu wa mradi. Watu wengi walikuwa na wasiwasi na hii ilikuwa mara ya kwanza ya kwamba mpango wa serikali ya China ilikubaliwa na 2/3 za wabunge pekee (kura 1767 za ndiyo, 177 za hapana na 664 za upande wowote). Baadaye maoni ya upimzani yalipihwa marufuku na wapinzani kadhaa walifungwa gerezani.

Ujenzi ulianza mwaka 1994 na bwawa likajaa mwaka 2008. Ualishaji wa umeme ulianza 2009.

Matatizo ya mradi

[hariri | hariri chanzo]

Sababu za wasiwasi na upinzani ulioendelea hadi mwisho ni kama vile:

  • uhamiaji wa watu milioni 1.24 ambao makazi yao wamefunikwa na maji ya bwawa jipya
  • uharibifu au angalau mabadiliko makubwa katika hifadhi ya taifa Mangenge Matatu
  • hatari kwa mazingira na upotevu wa aina kadhaa za wanyama waliohifadhiwa
  • hatari ya kujaza kwa bwawa kwa matope mtoni usiweza kuendelea kwenye njia ya mto na kuweza kujaza bwawa hivyo kupunguza faida ya lambo
  • hatari kwa ekoljia ya mazingira zisizojulikana maana haiwezekani kujua mabadiliko yote yanayofuatana na ujenzi wa lambo kubwa hivi

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:CommuniaCat

30°49′23″N 111°00′12″E / 30.82306°N 111.00333°E / 30.82306; 111.00333