Mafuriko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mafuriko katika eneo la TAZARA, Dar es Salaam, Tanzania
Mafuriko ya mto Elbe mjini Dresden, Ujerumani
Mafuriko huko Jangwani jijini Dar es Salaam, Tanzania

Mafuriko ni hali ya kuwa na maji mengi yanayofunika nchi kavu isiyo na maji kwa kawaida.

Mafuriko yanaweza kutokea

  • popote baada ya mvua kali inayoteremsha maji mengi yasiyo na njia ya kupotea, hasa baada ya kutelemka penye mlima au mtelemko
  • kando ya mto ama baada ya mvua kali au wakati wa mvua nyingi au kwenye majira ya kuyeyuka kwa theluji
  • kando ya ziwa au bahari kama upepo mkali unasukuma maji kuelekea pwani, hasa pamoja na kutokea kwa maji kujaa au bamvua

Mafuriko mara nyingi ni hatari kwa binadamu, huleta hatari kwa uhai, mali na nyumba.

Njia za kujiokoa ni pamoja na kuhama haraka sehemu za mabondeni kwenda penye miinuko au nchi ya juu zaidi. Watu waliozoea mafuriko wana mbinu za pekee kama vile kujenga vizuizi vya maji kupanda juu, kuchimba mifereji inayopeleka maji mbali au kujenga nyumba juu ya vilima wakijua hakuna njia ya kuzuia mafuriko.

Vifaa vya dharura vinavyohitajika[hariri | hariri chanzo]

Inafaa kuweka nyumbani kwako vifaa vinavyoweza kuhitajika katika kipindi cha dharura. Kwa kiasi, vifaa hivi vinafaa kuwa:

  • Vyombo safi kadhaa vya maji, vikubwa kutosha maji ya siku 3-5 (takriban galoni tano kwa kila mtu).
  • Ruzuku ya siku 3-5 ya chakula kisichoharibika haraka na kifungua mkebe kisichotumia umeme.
  • Vifaa vya huduma ya kwanza na kitabu cha mwongozo na maagizo ya matumizi ya dawa na mahitaji maalum ya kimatibabu.
  • Redio inayotumia betri, tochi, na betri za ziada.
  • Mifuko ya kulalia au blanketi za ziada.
  • Vifaa vya kusafisha maji, kama vile klorini au tembe za aidini au dawa ya klorini ya kawaida ya nyumbani isiyo na harufu.
  • Chakula cha mtoto na/au chakula kilichotayarishwa, nepi, na vifaa vingine vya mtoto.
  • Vitambaa vya kusafisha vya kutupika, kama “vipanguzi mtoto”vya kutumiwa na familia nzima iwapo vifaa vya kuogea havipatikani.
  • Vifaa vya usafi wa kibinafsi, kama sabuni, dawa ya meno, sodo, na kadhalika.
  • Mfuko wa vifaa vya dharura wa gari lako ukiwa na chakula, vitanui, kebo za kuongeza nguvu, ramani, vyombo, vifaa vya huduma ya kwanza, kizima moto, fuko la kulalia, na kadhalika.
  • Buti za mpira, viatu vyenye nguvu, na glavu zisizoingiza maji.
  • Kiwinga wadudu kilicho na DEET au Picaridin, visitiri, au mavazi yenye mikono na miguu mirefu ya kujikinga dhidi ya mbu wanaoweza kujikusanya kwa maji yanayosalia baada ya mafuriko. (Habari zaidi kuhusu hizi na viwinga vingine vinavyopendekezwa inaweza kupatikana fomu ya kisasa ya kanuni yenye Habari Kuhusu Kiwinga wadudu.

Matangazo kwa umma[hariri | hariri chanzo]

Iwapo umeamrishwa kuhama[hariri | hariri chanzo]

Usikose kutii amri ya kuhama. Mamlaka zitakuamrisha utoke iwapo uko katika eneo lililo chini, au katika sehemu yenye uwezekano mkubwa wa maji kupanda. Iwapo onyo ya mafuriko itatolewa katika eneo lako au uamrishwa na mamlaka kuhama:

  • Beba vitu muhimu tu.
  • Iwapo una wakati, zima gesi, umeme , na maji.
  • Toa plagi za vifaa vya umeme ili kuzuia madhara ya umeme unaporudi.
  • Fuata njia zilizotengwa za kuhama na utarajie msongmano mkubwa wa magari.
  • Usijaribu kuendesha gari au kutembea kwenye hori au barabara zilizofurika.

Ukiamrishwa kutohama[hariri | hariri chanzo]

Kujitunza katika mvua kubwa kwa njia salama zaidi:

  • Fuatilia matangazo ya redio au televisheni kuhusu hali ya anga.
  • Jitayarishe kuhamia kimbilioau nyumba ya jirani iwapo makazi yako yameharibiwa, au iwapo umeambiwa kufanya hivyo na mhudumu wa mambo ya dharura.

Kuzuia kuvu[hariri | hariri chanzo]

Maji ya mvua au ya mafuriko yanapoingia kwenye jengo lako, chukua hatua kuzuia ukuaji wa kuvu. Safisha na ukaushe vitu vilivyoloa katika saa 48 hadi 72. Hakikisha hewa safi inapita vizuri kwenye sehemu zilizoloa. Tupa vitu vilivyoloa ambavyo haviwezi kukarabatiwa. Ukiona au kunusa kuvu, ioshe kwa mmumunyo wa kikombe 1 cha dawa ya klorini ya nyumbani kwa galoni 1 ya maji.

Kutoa kuvu baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Hiki ni kidokezo kuhusu kutoa kuvu. Unaweza kusafisha kiasi kidogo cha kuvu wewe mwenyewe. Tumia mmumunyo wa kikombe 1 cha dawa ya klorini kwa galoni 1 ya maji. Yaani kikombe 1 cha dawa ya klorini – kwa galoni 1 ya maji.

Kumbuka, usichanganye dawa ya klorini au bidhaa zilizo na dawa ya klorini -- na amonia -- au bidhaa zilizo na amonia. Soma kitambulisho kwenye bidhaa yoyote ili uone kilicho ndani.

Kuzuia majeraha ya msumeno wa mnyororo baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Iwapo ni lazima utumie msumeno wa mnyororo, fuata maagizo ili uwe salama. Vaa kofia ngumu, miwani ya kujikinga, vizibo vya sikio, glavu nzito za kazi, na buti. Kila wakati shika msumeno katika kiwango cha kiuno au chini, na uhakikishe wengine wako mbali. Ukijikata, bana kidonda ili kukomesha kutoka kwa damu na upate usaidizi wa kimatibabu haraka iwezekanavyo.

Kunawa mikono baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mvua kubwa, maji chafu yanaweza kukufanya wewe na familia yako kuwa wagonjwa. Kumbuka kunawa mikono yako kwa sabuni na maji safi! Nawa mikono yako mara kwa mara, hasa kabla ya kutayarisha chakula, kabla ya kula, baada ya kutumia choo, na baada ya kusafisha. Kunawa mikono yako ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia maradhi.

Usalama wa umeme[hariri | hariri chanzo]

Kuzimika kwa umeme na mafuriko vinaweza kusababisha hatari za kielectriki. Usiguze waya ya umeme iliyo chini au chochote kilichoguzana nayo. Waya ya umeme ikiangukia gari lako, kaa ndani isipokuwa gari lishike moto au mamlaka ikushauri utoke nje. Usiguze mtu aliyeuawa na stima bila kuhakikisha kuwa mtu huyo hajaguzana na chanzo cha stima hiyo.

Kukaa salama karibu na majengo yaliyoharibiwa baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya tufani, kaa mbali na majengo yaliyoharibiwa hadi wakaguzi wa majengo watakaposeme yako salama kuingia. Inapokuwa salama, ingia tu wakati wa mchana ili uweze kuona hatari. Vaa mavazi ya kujizuia wakati wa kusafisha, na uepuke kupitia kwenye maji ili kupunguza majeraha. Toka mara moja unaposikia sauti zisizo za kawaida

Kuzuia pepopunda baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Unaposafisha baada ya mkasa, kuwa mwangalifu kwa mikato na vidonda. Kuzuia maambukizi, ikiwa ni pamoja na tetanasi, safisha mikato na majeraha yote kwa sabuni na maji safi, tumia lihamu ya antibiotiki na ufunike. Kidonda kikivimba au kutoa kioevu, tafuta matibabu mara moja

Majengo yaliyoharibiwa[hariri | hariri chanzo]

Ingia katika majengo yaliyoharibiwa wakati wa mchana ili uweze kuona hatari zozote. Vaa mavazi ya kujikinga kama glavu, miwani ya kujizuia na buti wakati wa kusafisha. Funika pua na mdomo ili uepuke kuvuta vumbi. Kuwa mwangalifu unaposongesha nyenzo na kifusi-- vitu vinaweza kusonga au kuanguka na kukujeruhi. Toka kwenye jengo hilo mara moja unaposikia sauti zisizo za kawaida. Vidokezo hivi vinaweza kuokoa maisha....Kuwa salama.

Cha kufanya iwapo vifaa vyako vina majimaji baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Moto wa nyumbani ni tishio baada ya mkasa wa asilia. Huenda malori ya kuzima moto yasiweze kulifikia boma lako kwa urahisi. Iwapo boma lako limefurika, tafuta ishara zinazoonyesha kuwa vifaa vyako vimeloa na uvitupe ili kujikinga dhidi ya mshtuko au moto. Tafuta mtaaluum achunguze boma lako na abadilishe vidhibiti gesi, vipima umeme na fyuzi zilizoloa wakati wa mafuriko.

Chakula salama na kisichowekwa katika friji[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mvua kubwa au mkasa, ni muhimu kula chakula salama tu. Tupa vyakula vinavyoharibika haraka, kama nyama, kuku, samaki, mayai na mabaki yaliyohifadhiwa kwa zaidi ya digrii 40 kwa saa 2 au zaidi. Tupa chakula kilicho na harufu, rangi, au sura isiyo ya kawaida. Tupa chakula ambacho labda kimeguzana na maji ya mafuriko, kikiwemo chakula katika mikebe iliyofura, iliyoboka na iliyoharibika. Unapokuwa na shaka, kitupe

Chakula salama[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mvua kubwa sana au mkasa asilia, ni muhimu kuhakikisha chakula chako kiko salama. Safisha mikono yako, na vyombo vinnavyotumiwa kutayarisha na kupakua chakula kwa maji kutoka katika vyanzo salama

Kuweka au kutupa chakula cha kubeba baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Usile chochote ambacho kimeguzana na maji ya mafuriko. Tupa vyombo vilivyo na vifuniko vya parafujo, vifuniko vya kupinda, vifuniko vya kugeuza, chakula cha mkebe cha nyumbani au chupa za soda za kiasilia za nyumbani zenye vifuniko vya kusokota iwapo maji ya mafuriko yaliguzana navyo. Usile chakula kilichowekwa au kufungwa na plastiki, kadibodi, kitambaa au vitu vingine kama hivyo au vyombo vilivyoguzana na maji ya mafuriko

Jinsi ya kusafisha mikebe ya chakula baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mafuriko, vitu vingine vya kula na kunywa si salama na lazima vitupwe. Lakini vyakula ambavyo havijaharibiwa vya kutayarisha vilivyo kwenye mikebe ya chuma vinaweza kufanywa salama. Toa vitambulisho, safisha kabisa, suuza, na uue vimelea kwenye vyombo hivyo kwa mmumunyo wa kusafisha wa kikombe kimoja cha dawa ya klorini kwa galoni moja ya maji. Weka vitambulisho tena na pia tarehe ya mwisho kutumika.

Dawa zilizotangamana na maji[hariri | hariri chanzo]

Bidhaa za dawa zilizotangamana na maji ya mafuriko au maji yoyote chafu zinaweza kuchafuliwa na zinapaswa kutupwa. Chunguza kwa makini dawa zako zote kama zimechafuliwa na maji zikiwemo dawa zilizotolewa katika pakiti zake za kawaida na kuwekwa katika viandalizi vya tembe au vyombo vingine. Tupa dawa zozote ambazo huenda zimechafuliwa, zikiwemo tembe, vimiminiko, dawa za sidano, vivutia hewa, na dawa za ngozi.

Dawa za kuokoa uhai[hariri | hariri chanzo]

Badilisha dawa zote za kuokoa uhai unazofikiri zimeharibika katika mkasa haraka iwezekanavyo. Katika dharura, unaweza kutumia dawa za kuokoa maisha zilizowekwa vizuri katika vyombo vyao iwapo zinaonekana za kawaida na kavu. Kumbuka kuacha kuzitumia mara tu dawa za kubadilisha zinapopatikana. Tupa tembe zozote zinazoonekana zimeloa au kuonekana na kunuka tofauti.

Kuhakikisha usalama wa watoto dhidi ya kuzama majini katika sehemu zilizofurika[hariri | hariri chanzo]

Mchakato wa kusafisha unapoanza baada ya mkasa asilia, kunaweza kuwa na sehemu za kufurika. Wachunge watoto wako kila wakati ili wasichezee ndani au karibu na maji. Haichukui muda mrefu wala maji mengi kwa watoto wadogo kuzama. Katika visa vingi, watoto waliozama walikuwa hawaonekani zaidi ya dakika tano na walikuwa chini ya utunzaji wa mzazi mmoja au wote wakati huo.

Kuzuia blista kwa miguu[hariri | hariri chanzo]

Blista kwa miguu hutokea miguu ikiloa kwa muda mrefu. Blista husababisha kuuma, kuvimba na uzito kwenye miguu. Kinga miguu yako — osha na ukaushe miguu yako; vaa soksi safi, kavu; lowanisha miguu iliyoathiriwa katika maji vuguvugu kwa dakika 5. Inua miguu unapolala. Tafuta matibabu mara moja unaposhuku mtu ana blista kwa miguu.

Utambuzi na matibabu ya hipothemia inayohusiana na kutangamana na maji baridi[hariri | hariri chanzo]

Kusimama au kufanyia kazi ndani ya maji baridi husababisha kupoteza joto la mwili haraka, na matokeo yake ni hipothemia. Punguza hatari ya hipothemia — vaa buti za mpira, hakikisha mavazi na buti zimehami vizuri, epuka kufanya kazi pekee yako, pumzika mara kwa mara nje ya maji, na ubadilishe uvae nguo kavu inapowezekana. Tafuta matibabu mara moja unaposhuku hipothemia.

Kuishi salama karibu na mbwa baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Mbwa wanaweza kuhofia na kufadhaika baada ya mkasa wa asilia na wanaweza kuuma au kukwaruza kwa urahisi. Usikaribie mbwa usiyemjua, na usisonge mbwa yeyote anapokukaribia. Epuka kuangaliana ana kwa ana, na usisumbue mbwa anayelala, anayekula, au anayetunza watoto wake. Watoto wasicheze na mbwa bila idhini ya mwenyewe na uangalizi wa mtu mzima.

Kudhibiti wanyama wagugunaji baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mkasa asilia, wanyama wagugunaji walionusurika kama vile panya huhamia sehemu mpya kutafuta chakula, maji, na makazi. Panya wanaweza kueneza magonjwa, kuchafua chakula, na kuharibu mali. Weka chakula katika vyombo vilivyofunikwa vilivyo na vifuniko vinavyoshika kabisa. Weka chakula, maji na vitu ambapo wanyama wagugunaji wanaweza kujificha mbali na wanyama hao.

Kuendesha gari katika maji baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mvua kubwa, barabara nyingi zinaweza kufurika. Epuka kuendesha gari kwenye maeneo haya, hasa maji yanapopita kwa kasi. Kuzama kunaweza kutokana na kuendesha gari kwenye maji. Kwa kweli, maji kidogo kama inchi sita yanaweza kukufanya upoteze udhibiti wa gari lako, na maji kidogo futi mbili yatabeba mengi ya magari madogo.

Kustahimili huzuni na mawazo ya kujiua baada ya mkasa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya mkasa asilia, ni kawaida kuhisi masikitiko, mwenye wazimu au hatia—huenda umepoteza vitu vingi sana. Iwapo unahisi kukata tamaa kabisa au mwenye mawazo ya kujiua, tafuta usaidizi. Kuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara na jamaa na marafiki, tafuta mfumo wa usaidizi, na uongee na mshauri. Kuwa na karibu na wengine kunaweza kusaidia

Maafa kutokana na mafuriko[hariri | hariri chanzo]

Hapo ni orodha ya mafuriko yanayojulikana kuleta maafa mengi.

Idadi ya vifo Tokeo Mahali Mwaka
2,500,000–3,700,000[1] Mafuriko ya China 1931 China 1931
900,000–2,000,000 Mafuriko ya Hwangho 1887 China 1887
500,000–700,000 Mafuriko ya Hwangho 1938 China 1938
231,000 Kuvunjika kwa mlambo wa Banqiao; takriban watu 86,000 walikufa kutokana na mafuriko na wengine 145,000 kutokana na magonjwa yaliyofuata China 1975
230,000 Tsunami kwenye Bahari Hindi 2004 Indonesia, Uhindi, Sri Lanka 2004
145,000 Mafuriko ya Yangtze 1935 China 1935
zaidi ya watu 100,000 Mafuriko ya Uholanzi 1530 Netherlands 1530

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Worst Natural Disasters In History. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-04-21. Iliwekwa mnamo 2010-07-28.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: