Nenda kwa yaliyomo

Dresden

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majengo mazuri ya Dresden yalitengenezwa upya baada ya maangamizi ya 1945
Mahali pa Dresden katika Ujerumani

Dresden ni mji mkuu wa jimbo la Saksonia katika Ujerumani mwenye wakazi 484,700. Uko kando la mto Elbe.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Dresden ilikuwa mji muhimu kama makao makuu ya wafalme wa Saksonia waliojenga jumba la kifalme na makanisa mazuri.

Mwishoni wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mji ukaharibiwa kabisa katika mashambulio ya jeshi la anga la Uingereza yanayojulikana kama maangamizi ya Dresden. Mji ulijaa wakimbizi kutoka sehemu za mashariki ya Ujerumani na takriban watu 35,000 walikufa katika siku tatu kati ya 13 na 15 Februari 1945.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dresden kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.