Nenda kwa yaliyomo

Tsunami

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Watu wakikimbia wimbi la tsunami tarehe 26 Desemba 2004 lilipogonga mwambao wa Ao Nang nchini Uthai.

Tsunami ni wimbi kubwa sana katika bahari linalosababishwa na tetemeko la ardhi, mlipuko wa volkano au matokeo mengine yanayoleta mshtuko wa ghafla chini ya maji. Mshtuko huo unasababisha kutokea kwa wimbi kali linaloanza kupaa juu likifika katika maji kame na kwenye ufuko wa bahari.

Neno tsunami linatokana na lugha ya Kijapani likimaanisha "wimbi la bandarini".

Tsunami huweza kutokea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Wakati mwingine inaweza kutokea bila kuleta madhara yoyote.

Tsunami ya Krismasi 2004

[hariri | hariri chanzo]
Uenezi wa mawimbi ya tsunami wa Krismasi 2004 katika Bara Hindi

Tsunami ya Krismasi 2004 ilikuwa mojawapo kati ya maafa makubwa yaliyotokea katika historia ya dunia yetu iliyoua malakhi ya watu huko Asia Kusini na kuleta madhara hadi pwani ya Afrika ya Mashariki.

Tarehe 26 Desemba 2004 lilitokea tetemeko la ardhi chini ya Bahari Hindi karibu na pembe ya kaskazini ya Sumatra kwenye mstari ambako bamba la Uhindi linajisukuma chini ya bamba dogo la Burma. Siku ile km 1,200 za pembizo la bamba la Uhindi zilisogea mbele katika muda wa dakika chache kwa urefu wa takriban mita 15 chini ya bamba la Burma. Bamba la juu lilisukumwa na kupaa juu hadi mita 30. Mshtuko huo ulianzisha wimbi kubwa chini ya bahari lililotoka juu kwa umbo la tsunami iliyoua takriban watu 275,000.

Katika maji marefu ya bahari wimbi halikuwa na hasara likaonekana kuwa na cm 30 pekee. Lakini ilifika mwambaoni kwenye maji kama likaanza kupaa juu kufikia hadi m 30.

Kutoka kitovu cha tetemeko la ardhi mawimbi ya tsunami yalienea kotekote. Yalipiga vikali sana pwani za Indonesia, Sri Lanka, Thailand na India. Mawimbi yalifikia hadi pwani ya Afrika na kusababisha vifo Somalia, Kenya, Tanzania na Afrika Kusini.

Athari za tsunami kwa afya

[hariri | hariri chanzo]
 • Baada ya kuokoa watu, jambo la msingi kwa afya ya umma ni kusafisha maji ya kunywa, chakula, makazi, na utunzaji wa majeraha.
 • Maji ya mafuriko yanaweza kuleta hatari za kiafya kama vile maji na vyakula vilivyochafuliwa.
 • Upotezaji wa makazi huwaacha watu katika hali ya kutangamana na wadudu, joto na hatari zingine za kimazingira.
 • Vingi vya vifo vinavyohusiana na tsunami husababishwa na kuzama, lakini majeraha ya kisaikolojia ni tatizo la msingi pia. Majeraha kama vile kuvunjika mikono au miguu na majeraha ya kichwa husababishwa na athari za kimwili za watu wanaosukumwa na maji kwenye vifusi kama vile nyumba, miti na vitu vingine visivyosonga. Maji yanapopungua, uvutaji na uondoaji wa vifusi kwenye maeneo yaliyo na watu wengi unaweza kusababisha majeraha zaidi na kudhoofisha majengo na huduma.
 • Utunzaji wa kimatibabu ni muhimu sana katika maeneo ambapo kuna huduma finyu ya afya.

Madhara ya baadaye

[hariri | hariri chanzo]
 • Mikasa ya kiasili haisababishi ongezeko la magonjwa ya kuambukiza katika mkurupuko. Hata hivyo, maji na vyakula vilivyochafuliwa na aidha ukosefu wa makazi na huduma ya afya vinaweza kuwa na madhara ya baadaye ya kukithiri kwa maradhi yaliyo kwenye sehemu iliyoathiriwa.
 • Miili inayooza husababisha hatari ndogo sana ya mkurupuko mkuu wa ugonjwa.
 • Watu walio hatarini zaidi ni wale wanaoshughulikia miili au kuiandaa kwa mazishi.

Athari za mkasa hudumu kwa muda mrefu. Mahitaji makuu ya kifedha huwa miezi ya mkasa, yakiwemo:

 • ukaguzi na ufuatiliaji wa magonjwa ya kuambukiza na yanayosambazwa na maji au nzi;
 • ugeuzaji wa vifaa vya matibabu kutoka sehemu zisizoathiriwa ili kukidhi mahitaji ya sehemu zilizoathiriwa;
 • udumishaji wa huduma za afya za kimsingi, mifumo ya maji, makazi, na ajira; na
 • kusaidia jamii kurejea katika hali ya kawaida kisaikolojia na kijamii baada ya mkasa.

Usalama wa chakula baada ya tsunami

[hariri | hariri chanzo]

Ili kuzuia magonjwa yanayotokana na chakula, nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kula au kutayarisha chakula na baada ya kutumia choo au bafu. Iwapo huna maji safi, tumia visafisha mikono visivyo na maji hadi maji safi yatakapopatikana.

Usile chakula chochote ambacho hakijahifadhiwa kwenye vyombo visivyoingiza maji (vyombo vya mikebe au vya plastiki vilivyofungwa) na kile ambacho huenda kimetangamana na maji yasiyotibiwa, kama vile maji ya bahari, mafuriko, mto au dimbwi. Tupa chakula chochote kilicho katika mikebe isiyofungwa au inayoingiza maji ambacho kimetangamana na maji yasiyotibiwa.

Vyakula vya mikebe ambavyo havijaharibika vinaweza kuokolewa. Ondoa vitambulisho kwenye mikebe, safisha sehemu ya nje ya mikebe hiyo kwa maji ya sabuni, na uue viini kikamilifu kwenye mikebe hiyo kwa mchanganyiko wa kikombe 1 (aunsi 8; takribani lita 0.25) cha klorini (asilimia 5.25) katika galoni 5 (takribani lita 19) za maji safi yaliyotibiwa. Tumia kalamu kuandika yaliyomo na tarehe ya kuharibika kwenye mikebe hiyo.

Iwapo mikebe ya chakula iliyofunguliwa ina vifuniko vyenye hesi, meno, vilivyokunjwa (vifuniko vya chupa za soda), vilivyopinda, au vya kubingirika, au ikiwa imetengenezwa nyumbani, itupe ikiwa imetangamana na maji ambayo hayajatibiwa. Haiwezi kutiwa kiua viini.

Ikiwa hunyonyeshi, katika kulisha watoto wachanga tumia chakula cha mtoto kilichotengenezwa na kuhifadhiwa mikebeni kisichohitaji kuongezwa maji.

Ikiwa barafu kavu itapatikana, inaweza kutumiwa kudumisha ubaridi wa chakula — pauni 25 (takribani kilogramu 11.5) za barafu kavu zitadumisha friza ya futi 10 (lita 283) chini ya kiwango cha kuganda kwa siku 3 hadi 4.

Kuwa makini unaposhughulikia barafu kavu, kwa sababu hugandisha kila inachogusa. Vaa glavu kavu na nzito ili kuepuka majeraha. Barafu kavu inapoyeyuka hubadilika kutoka hali ngumu na kuwa gesi.

Pitisha hewa safi (ondoa hewa) kwenye magari au vyumba unaposafirisha, kuhifadhi au kutumia barafu kavu. Bila kupita kwa hewa safi, gesi inayotoka kwenye barafu inayoyeyuka inaweza kuongezeka polepole na kusababisha madhara, yakiwemo kupoteza fahamu na kifo.

Tatizo la maji baada ya tsunami

[hariri | hariri chanzo]

Tsunami inaweza kutengeneza mbingiriko wa maji ya bahari ambayo inaweza kutapakaa sehemu kubwa ya kijiografia. Maji ya bahari yakiendelea kusongea ufuoni, maji ya kunywa ya visima yanaweza kuzamishwa na kuweza kuchafuliwa na vidubini (bakteria, virusi, parasiti) na kemikali ambazo zinaweza kuathiri afya ya binadamu. Chumvi ya baharini inayohusishwa na maji ya chumvi inayofurika maji ya kunywa ya pwani si tishio la haraka kwa afya.

Kwa sababu ya ladha mbaya ya maji ya chumvi, watu wengi hawawezi kumeza (kunywa) maji mengi: hiyo itasababisha shida za afya mara moja. Hata hivyo, ugonjwa unaosababisha vidubini husambaa kupitia mafuriko kwa kawaida huwa haitoi ladha nzito. Ikiwa maji yaliyona ugonjwa-yanayosababisha vidubini yatanyiwa, hata kwa kiwango kidogo, inaweza kusababisha shida za afya kwa maisha kama vile uharishaji ulio sugu, kipindupindu, na maambukizi hatari. Matumizi ya maji chafu kusafisha vidonda yanaweza kuleta maambukizi hatari.

Zaidi ya hayo, uchafu wa kemikali unaopatikana katika mafuriko ya maji unaweza kuchafua visima kwa urahisi. Uchafu wa kemikali unaweza kujumuisha bidhaa za fueli kutoka kwa tangi za fueli zilizoanguka, au dawa za kuua wadudu ambazo zimehifadhiwa katika meneo ya mafuriko. Ukinywa maji yaliyo na aina hii ya uchafu wa kemikali inaweza kuwa hatari kwa afya na maisha.

Baada ya visima kusafishwa vizuri na kuanza kujaza maji kutoka kwa mpenyo wa mwamba, kiwango kikubwa cha chumvi (kuwa na chumvi nyingi) unapaswa kupungua. Visiwa vifupi vinaweza kuathiriwa zaidi kuliko visima vyenye kina ndefu kwa sababu ya kuwepo kwa maji ya chumvi katika eneo la juu ya udongo. Ingawa kuanza upya kwa visima vinaweza kuwa pole pole kuliko ile ya visima vyenye kina ndefu, kuwepo kwa chumvi kwa visima vinapaswa kuwa kidogo kwa muda.

Baada ya tsunami, watu katika sehemu zilizoathirika wanapaswa kusikiza matangazo ya umma kuhusu usalama wa kupeana maji. Visima vya kibinafsi vilivyofurika vinapaswa kuchunguzwa na kusafishwa baada ya maji ya mafuriko kupungua. Ikiwa harufu mbaya, ladha na rangi isiyo kuwa ya kawaida, au matokeo ya awali ya uchunguzi wa maji yatafanya watu washuku kuwa visima vya eneo hilo vimechafuliwa na fueli, dawa ya kuua wadudu, au hata kemikali zingine, uchunguzi wa kemikali ya maji ya kunywa unahitaji sana. Maswali kuhusu uchunguzi yanapaswa kutolewa kwa viongozi wa eneo hilo.

Maji mazuri ya kunywa, kupikia, na usafi wa kibinafsi inajumuisha maji yaliyowekwa kwa chupa, chemshwa, au kutibiwa. Baada ya tsunami, asili ya maji yanaweza kuchafuliwa na maji ya chumvi. Ukitumia maji ya chumvi (mchanganyiko wa maji ya chumvi na maji isiyotiwa chumvi) kwa kunywa na kupika kwa muda mrefu yanaweza kusababisha shida za afya kutoka kwa viwango vya juu ya chumvi yanayoweza kunyiwa. Viongozi wa eneo lako wanaweza kupanga mapendekezo maalum kwa uchemshaji na uwekaji wa kemikali maji katika eneo lako. Ukipata maji kutoka kwa tangi la maji au kisima, tafadhali rejelea ujumbe wa kusafisha matangi ya maji au visima. Usipopata maji kutoka kwa tangi la maji au kisima, fuata sheria hizi kuhusiana na maji ya kunywa, kupikia, na usafi wa kibanfsi.

Mashauri muhimu

[hariri | hariri chanzo]
 • Usitumie maji yaliyochafuliwa kuosha vyomba, kusugua meno, kuosha na kutayarisha chakula, kuosha mikono, kutengeneza barafu au kutayarisha fomyula ya mtoto. Ikiwezekana, tumia fomyula ya mtoto isiyohitaji kuongezwa maji. Unaweza kutumia kisafisha mikono chenye alkoholi ili kuosha mikono.
 • Ikiwa utatumia maji ya chupa, hakikisha kuwa yametolewa katika chanzo salama. Ikiwa hujui iwapo maji hayo yalitolewa kwenye chanzo salama, unapaswa kuyachemsha au kuyatibu kabla ya kutumia. Tumia maji ya chupa, yaliyochemshwa au yaliyotibiwa tu hadi maji ya chanzo chako yatakavyochunguzwa na kupatikana kuwa salama.
 • Kuchemsha maji, kunapowezekana, ndiyo njia bora zaidi ya kuua bakteria na parasiti. Kuchemsha maji kwa dakika 1 kutaua vimelea vingi. Hata hivyo, kuchemsha maji ya chumvi kwa zaidi ya dakika 5 kunaweza kuongeza kukolea kwa chumvi za bahari na vichafuzi vingine.
 • Iwapo hautaweza kuchemsha maji, unaweza kuyatibu kutumia tembe za klorini, aidini au dawa ya klorini ya nyumbani isiyo na harufu (asilimia 5.25 ya sodium hypochlorite):
 • Ukitumia tembe za klorini au aidini, fuata maagizo yanayokuja na tembe hizo.
 • Ukitumia dawa ya klorini ya nyumbani, ongeza 1/8 ya kijiko cha chai (takriban mililita 0.75) ya klorini kwa kila galoni ya maji ikiwa maji haya ni safi. Kwa maji yasiyo safi, ongeza 1/4 ya kijiko cha chai (takriban mililita 1.50) ya klorini kwa kila galoni. Changanya mmumunyo huu kikamilifu kisha uuache kwa dakika 30 kabla ya kutumia.
 • Fahamu: Kutibu maji kwa tembe za klorini, aidini au dawa ya majimaji hakutaua parasiti.

Tumia mmumunyo wa dawa ya klorini kukamua vyombo vya maji kabla ya kuvitumia tena. Tahadhari unapotumia tangi za kuhifadhi maji na aina zingine za vyombo. Kwa mfano, tangi za maji za zimamoto na makopo au chupa zilizotumika awali huenda zimechafuliwa na mikrobu au kemikali. Usitegemee matumizi ya vyombo ambavyo havijajaribiwa vya kusafisha maji.

Kuua viini vya maradhi kwenye Matangi ya Maji na Mifumo Mingine ya Kunasa Maji ya Mvua Baada ya Mafuriko

Katika maeneo mengi ulimwenguni, watu hupata maji ya kunywa kwenye mifumo ya kunasa (kukusanya) maji ya mvua na kuyahifadhi. Hata inapotengenezwa na kutumika inavyofaa, mifumo hii huchafuliwa kwa urahisi na viinitete vinavyoweza kusababisha magonjwa. Baadhi ya mifumo ya kusambaza maji hutumia sehemu kama vile paa ili kukusanya maji na kuyaelekeza kwenye tangi la maji (tangi la kuhifadhi). Ikiwa hupati maji yako kutoka kwa tangi au kisima, rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na Usafi wa Kibinafsi kwa habari kuhusu kuua viini kwenye maji yako.

Maji ya matangi ya maji na mifumo sawa yanapotangamana na maji ya mafuriko, watu wanapaswa kuchukulia kuwa maji yao ya kunywa yamechafuliwa. Ikiwa unasikitika kuhusu kuchafuliwa kwa chanzo cha maji yako ya kunywa, tafadhali rejelea Maji ya Kunywa, Kupika, na Usafi wa Kibinafsi kuhusu uchafuzi wa maji chumvi, uchafuzi wa kemikali na athari za kiafya.

Moja ya mbinu zifuatazo inaweza kutumika kuua viini kwenye matangi ya maji na mifumo mingine ya kunasa maji ya mvua katika hali za mikasa kwa kuzingatia iwapo chanzo cha maji ya kunywa kinapatikana tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unasafishwa (Mbinu ya 1) au iwapo tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unahitaji kutumika kwa haraka zaidi kama chanzo cha maji ya kunywa (Mbinu ya 2). Iwapo bidhaa za fueli au vichafuzi vingine vya kemikali vimetangamana na tangi la maji au mfumo wa kunasa maji ya mvua, au iwapo kuna harufu ya fueli au kemikali zingine katika mazingira karibu na mfumo huo, tumia tu Mbinu ya 1 kwa uuaji viini.

Mbinu ya 1—Tumia mbinu hii ikiwa maji safi ya kunywa yanapatikana kutoka kwenye chanzo kingine tangi la maji au mfumo wa kunasa maji unaposafihshwa. Mbinu hii ni bora, lakini huchukua muda mrefu zaidi, kwani tangi la maji/mfumo ni lazima utolewe maji yote na kujazwa tena mara mbili.

 1. Safisha kikamilifu sehemu ya kunasa maji (kwa mfano, paa) na uondoe vifusi vyote.
 2. Ondoa maji kwenye tangi la maji kikamilifu.
 3. Ondoa vifusi vyote kwenye tangi.
 4. Bila kuingia kwenye tangi, sugua sehemu ya ndani vizuri iwezekanavyo kwa brashi dhabiti au ufagio na mmumunyo wa kikombe 1 (aunsi 8; takriban lita 0.25) wa asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu (sodium hypochlorite) katika galoni 10 (takriban lita 38) za maji.
 5. Jaza tena tangi hilo kwa maji ya mvua au kutoka kwenye chanzo kingine.
 6. Iwapo hufahamu kiasi cha tangi, tumia fomyula ifuatayo kutambua kiasi cha maji linachoweza kuhifadhi: Kwa tangi la umbo la mstatili, zidisha kina cha tangi (katika futi) kwa urefu (katika futi) na kwa upana (katika futi), kisha uzidishe matokeo kwa 7.5 ili kupata idadi ya galoni zitakazojaza tangi hilo. Kwa tangi la mviringo, zidisha urefu (katika futi) kwa matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe, zidisha matokeo kwa 3.14, na kisha uzidishe matokeo hayo kwa 7.5 ili kupata galoni. Ikiwa hakuna mbinu kati ya hizi inayoweza kutumika, unaweza kukadiria kiasi kwa galoni kwa kufanya "kisio la kidhahania," kisha uzidishe kiasi cha dawa itakayotumika mara mbili katika mmumunyo wa kuua viini.

Kipimo kwa mita: Katika vipimo vya mita, zidisha urefu (mita) X upana (mita) X kina (mita) X 1,000 = kiasi katika lita. Kwa matangi ya mviringo, zidisha kina X matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe (mita) X 3,140 = kiasi katika lita.

 1. Ongeza vikombe 4 (aunsi 32; takribani lita 1) vya asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu kwa kila galoni 100 (takribani lita 380) za maji katika tangi. Hii inapaswa kukupa ukolezi wa klorini wa takribani sehemu 100 kwa kila milioni.
 2. Fungua maji kwenye paipu zote zinazotumika kwa maji ya kunywa nyumbani kwako hadi utakapotambua harufu kali ya klorini.
 3. Wacha mmumunyo huo utulie kwa saa 24.
 4. Ondoa maji yote kwenye tangi.
 5. Jaza tangi kwa maji ya mvua au ulijaze kwa maji yanayoweza kunyweka.
 6. Foka paipu zote za nyumbani kwako hadi harufu ya klorini itakapoisha kabisa kabla ya kuanza kutumia mfumo huu tena.

Mbinu ya 2— Tumia mbinu hii ikiwa maji safi ya kunywa yanapatikana kutoka kwa asili nyingine wakati tangi/mfumo unaambukuliwa. Mbinu hii si bora kama ilivyo Mbinu ya 1, lakini huchukua muda mfupi kwani tangi/mfumo unahitaji kutolewa maji na kujazwa tena mara moja tu.

 1. Safisha kikamilifu sehemu ya kunasa maji (paa) na utoe vifusi vyote.
 2. Iwapo haufahamu kiasi cha tangi, tumia fomyula ifuatayo kutambua kiasi cha maji kinachoweza kuwekwa ndani ya tangi: Kwa tangi la mstatili, zidisha kina cha tangi (katika futi) kwa urefu (katika futi) na kwa upana (katika futi), kisha uzidishe matokeo na 7.5 ili kupata idadi ya galoni. Kwa tangi la mviringo, zidisha urefu (futi) kwa matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo kwa chenyewe, zidisha matokeo kwa 3.14, kisha uzidishe matokeo hayo kwa 7.5 ili kupata idadi ya galoni zinazoweza kulijaza. Ikiwa hakuna mbinu kati ya hizi inayoweza kutumika, unaweza kukadiria kiasi kwa galoni kwa kufanya "kisio la kidhahania," kisha uzidishe kiasi cha dawa itakayotumika mara mbili katika mmumunyo wa kuua viini. Kipimo kwa mita: Katika vipimo vya mita, zidisha urefu (mita) X upana (mita) X kina (mita) X 1,000 = kiasi katika lita. Kwa matangi ya mviringo, zidisha kina X matokeo ya kuzidisha nusu kipenyo cha tangi kwa chenyewe (mita) X 3,140 = kiasi katika lita.
 1. Ongeza vikombe 4 (aunsi 32; takribani lita 1) vya asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu kwa kila galoni 100 (takribani lita 380) za maji katika tangi. Hii inapaswa kukupa ukolezi wa klorini wa takribani sehemu 100 kwa kila milioni.
 2. Fungua maji kwenye paipu zote zinazotumika kwa maji ya kunywa nyumbani kwako hadi utakapotambua harufu kali ya klorini.
 3. Wacha mmumunyo huo utulie kwa saa 24.
 4. Ondoa maji yote kwenye tangi.
 5. Ondoa vifusi vyote kwenye tangi.
 6. Bila kuingia kwenye tangi, sugua vizuri sehemu ya ndani ya tangi kwa brashi dhabiti au ufagio na mmumunyo wa kikombe 1 (aunsi 8; takriban lita 0.25) wenye asilimia 5.25 ya dawa ya klorini isiyo na harufu (sodium hypochlorite) katika galoni 10 (takribani lita 380) za maji.
 7. Ondoa mmumunyo wote wa kiua viini kwenye tangi.
 8. Jaza tena tangi kwa maji.
 9. Foka paipu zote za nyumbani kwako hadi harufu ya klorini itakapoisha kabisa kabla ya kuanza kutumia mfumo huu tena.

Kuua viini kwenye visima

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya tsunami, huenda visima katika maeneo yaliyoathiriwa vikawa vimechafuliwa. Tafadhali rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na ya Usafi wa Kibinafsi kuhusu uchafuzi wa maji chumvi, uchafuzi wa kemikali na athari za afya. Iwapo unashuku kuwa kisima chako kimechafuliwa, wasiliana na mamlaka za eneo lako kwa ushauri mahususi zaidi. Iwapo haupati maji yako kutoka kwa tangi au kisima, rejelea Maji ya Kunywa, Kupika na ya Usafi wa Kibinafsi kwa habari kuhusu kuua viini kwenye maji yako. Yafuatayo ni baadhi ya maagizo ya jumla ya kuua viini kwenye visima.

Kuua viini kwenye Visima Vilivyotobolewa au Vilivyochimbwa

 1. Vuta maji yote kutoka kwa kisima. (Fahamu: Katika sehemu zisizo na nguvu za umeme, jenereta ya kubeba inaweza kuhitajika kuendesha pampu.) Tumia mifereji ya nje kuondoa maji kwenye kisima iwapo inapatikana.
 2. Tumia Jedwali 1 kukokotoa kiasi cha dawa ya klorini (kimiminiko au chembe) cha kutumia.
 3. Ili kubainisha kiasi kamili cha kutumia, zidisha kiasi cha kiua viini kinachohitajika (kulingana na kipenyo cha kisima) na kina cha maji kwenye kisima hicho. Kwa mfano, kisima chenye kipenyo cha futi 5 huhitaji vikombe 4½ vya dawa ya klorini kwa kila futi ya maji. Iwapo maji katika kisima hicho ni futi 30 kwenda chini, zidisha vikombe 4½ na futi 30 ili kubainisha idadi kamili ya vikombe vya dawa ya klorini vinavyohitajika (4½ X 30 = vikombe 135).

Mfumo wa mita: Katika mfumo wa mita, kisima chenye kipenyo cha takribani mita 1.5 huhitaji takribani lita 1.1 za dawa ya klorini kwa kila mita ya maji. Iwapo kisima ni takribani mita 9.1 kwenda chini, zidisha lita 1.1 na mita 9.1 ili kubainisha idadi kamili ya lita za dawa klorini itakayohitajika (1.1 X 9.1 = lita 10). Futi moja ya urefu wa maji = mita 0.305.

 1. Weka idadi hii kamili ya kiasi cha kiua viini katika galoni 10 za maji (lita 38). Rashia mchanganyiko huu kwenye ukuta au bitana ya kisima. Hakikisha kuwa kiua viini hicho kinagusa sehemu zote za kisima hicho.
 2. Funga kabisa sehemu ya juu ya kisima hicho.
 3. Fungua mifereji yote na uvute maji hadi utakapotambua harufu nzito ya dawa ya klorini kwenye kila mfereji. Kisha simamisha pampu na uwache mmumunyo huo kwenye kisima kwa saa 24 au, kwa kiwango cha chini, usiku kucha.
 4. Siku itakayofuata, endesha pampu kwa kufungua mifereji yote, kuendelea hadi harufu ya klorini itakavyoisha. Weka sawa mtiririko wa maji kwenye mifereji au vyombo vinavyopeleka maji kwenye mifumo ya maji chafu iweze kutiririka polepole ili kuepuka kujaza mno mfumo wa utupaji.

Kuua viini kwenye visima vilivyotoboka

[hariri | hariri chanzo]
 1. Foka kisima hadi maji yawe safi. (Fahamu: Katika maeneo yasiyo na stima, genereta inayoweza kusogezwa kutoka mahali pamoja hadi pengine itahitajika ili kutumia pampu.) Tumia mifereji ya nje kutoa maji kutoka kwa kisima ikiwa inapatikana.
 2. Tambua kiasi cha maji katika kisima kwa kuzidisha galoni kwa kila futi ya kina cha kisima kwa futi (Jedwali 2). Kwa mfano, kisima kilicho na kipenyo cha inchi 6 ina galoni 1.5 ya maji kwa kila futi. Ikiwa kina cha kisima hiki ni futi 120, zidisha 1.5 kwa 120 (1.5 X 120 = galoni 180).

Kipimo cha mita: Katika kipimo cha mita, tambua kiasi cha maji kwenye kisima kwa kuzidisha lita kwa kila mita kwa kina cha kisima kwa mita. Kwa mfano, kisima chenye kipenyo cha sentimita 15.2 kina lita 18.6 za maji kwa kila mita. Ikiwa kina cha kisima hiki ni mita 36.5, zidisha lita 18.6 kwa mita 36.5 ili kutambua idadi jumla ya lita za maji katika kisima (18.6 X 36.5 = lita 679).

 1. Kwa kila galoni 100 (lita 380) za maji kwenye kisima, tumia kiasi cha klorini (aina ya maji au chembechembe) kama ilivyoashiriwa katika Jedwali 3. Changanya kiasi chote cha klorini ya maji au chembechembe na takriban galoni 10 (lita 38) za maji.
 2. Weka mmumunyo katika eneo la juu la kisima kabla ya kufunika.
 3. Unganisha mpira wa maji kutoka kwa mfereji ambapo maji hutokea kwa tangi kwa kifuniko cha kisima. Endesha pampu. Nyunyiza maji ndani ya kisima na uoshe pande za kifuniko kwa angalau dakika 15.
 4. Fungua mfereji yote katika mfumo na uache maji yapite hadi utakaponusa klorini. Kisha funga mifereji yote na uzibe sehemu ya juu ya kisima.
 5. Acha kisima kwa saa 24, au kwa muda mchache zaidi, usiku kucha.
 6. Baada ya kuacha maji ndani ya kisima, endesha pampu kwa kufungulia mifereji yote na kuendelea hadi harufu ya klorini inapoisha. Sawazisha mwendo wa mifereji ya maji au chombo kinachotoa maji hadi kwa mifumo ya maji machafu hadi kufukia mwendo wa polepole ili kuepuka kuweka shinikizo katika mfumo wa maji machafu.

Usafi baada ya Tsunami

[hariri | hariri chanzo]

Ni muhimu kukumbuka kutekeleza usafi wa kimsingi katika kipindi cha dharura. Osha mikono kila mara yako kwa sabuni na maji yaliyochemshwa au yaliyotiwa kiua viini. Maji yaliyochemshwa ndiyo bora zaidi.

Mifano ya nyakati za kuosha mikono yako ni:

 • kabla ya kutayarisha au kula chakula;
 • baada ya kutumia choo;
 • baada ya kushiriki katika shughuli za kushafisha baada ya mafuriko; na
 • baada ya kushika vitu vilivyochafuliwa na maji ya mafuriko au maji taka.

Maji safi yasipopatikana, unaweza kutumia bidhaa zenye spiriti zilizotengenezwa kwa ajili ya kuosha mikono.

Maji ya mafuriko yanaweza kuwa na kinyesi kutoka kwa mifumo ya maji taka yanayoenea kwenye ardhi na mapato ya ziada ya kilimo na viwanda. Ingawa mgusano wa ngozi na maji ya mafuriko kwa wenyewe hauleti hatari kubwa ya afya, kuna hatari ya magonjwa kutokana na kula au kunywa chochote kilichochafuliwa na maji ya mafuriko. Ikiwa una vidonda wazi ambavyo vitatangamana na maji ya mafuriko, hakikisha umevisafisha vyema iwezekanavyo kwa kuviosha kwa sabuni ili kudhibiti maambukizi. Kidonda kikianza kuwa chekundu, kuvimba au kuwa na mtiririko, tafuta usaidizi wa kimatibabu mara moja.

Isitoshe, wazazi wanahitaji kuwasaidia watoto kuepuka maradhi yanayoenezwa na maji. Usiwaruhusu watoto kucheza katika maeneo yenye maji ya mafuriko, osha mikono ya watoto mara nyingi (kila mara kabla ya kula) na usiwaruhusu kuchezea vinyago vilivyochafuliwa na maji ya mafuriko ambavyo havijatiwa kiua viini. Unaweza kutumia mmumunyo wa kikombe kimoja cha klorini katika galoni 5 za maji kwa kuua viini kwenye vinyago. Vinyago vingine kama vile wanyama waliojazwa nguo na vinyago vya watoto haviwezi kutiwa kiua viini; vinapaswa kutupwa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tsunami kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.