Kidubini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vidubini)
Jump to navigation Jump to search
Kundi la bakteria za Escherichia coli zikikuzwa mara 10,000

Vidubini (ing. microorganism au microbe) ni jina kwa kundi la viumbehai vidogo sana. Kidubini hakionekani kwa macho bali kwa msaada wa kitambo kama hadubini pekee.

Kidubini ni nini?[hariri | hariri chanzo]

Vidubini ni kundi lenye tbia tofauti sana kati yao. Vingi vyao vina seli moja pekee lakini kuna pia vidubini vyenye seli kadhaa kama vile kuvu na algae. Tabia ya pamoja ni udogo pekee.

Aina za vidubini[hariri | hariri chanzo]

Kati ya vidubini kuna

Aina nne za kwanza zinaweza kuishi pekee zao au ndani ya miili ya viumbehai vingine. Virusi huzaa ndani ya viumbehai vingine pekee. [1][2][3]

Wataalamu wengine hawahesabu virusi kati ya vidubini kwa sababu si viumbehai kweli.

Upatikanaji wa vidubini[hariri | hariri chanzo]

Vidubini ni muhimu sana katika mchakato wa uhai; algae ya diatomi zinatekeleza sehemu kubwa ya usanisinuru duniani ambayo ni msingi kwa lishe ya mimea na wanyama wengi.

Vidubini vingine ni vidusia au pathojeni za magonjwa ya kuambukiza.

Kwa jumla idadi ya vidubini ni kubwa kabisa kuliko viumbehai vyote vingine na asilimia 70 za biomasi duniani ni vidubini. Maana viumbe hivi vidogo visivyoonekana kwa macho kwa pamoja ni vizito kushinda wanyama na mimea yote ya dunia.

Vidubini vinapatikana kila mahali pa dunia hata kwenye tako la bahari, ndani ya miamba ya ganda la dunia au kwenye ncha za milima marefu hata zikielea katika hewa.

Vidubini ni muhimu katika lishe ya viumbe vingine; vinatekeleza kazi ya kuozesha mata hai iliyokufa (mimea, maiti za wanyama) na kuibadilisha katika hali inayoweza kutumiwa na mimea.

Vidubini vinavyoishi pekee zao[hariri | hariri chanzo]

Vidubini visivyoishi ndani ya miili ya viumbehai vingine vinapata nishati yao kwa njia mbalimbali.

Vingi hutumia nishati ya nuru kwa njia ya usanisinuru, sawa na mimea. Vingine vinatumia kemikali asilia katika mazingira yao na vikitumia nishati inayopatikana kwa kuvunja muungo kemia ya kampaundi.

Vingine vinaishi kwa kuozesha mata hai iliyokufa kama majani yaliyoanguka na maiti za wanyama. Katika mazingira asilia mata iliyooza inachanganywa tena kwa na udongo na hivyo kurudisha Kwa njia hii vinarudisha virutubishi katika ardhi ambavyo vingepungua mno bila mchakato wa kuoza na kurudisha virutubisho.


Vidubini kama hamira ni muhimu kwa kutengeneza vyakula kama mkate, jibini, divai na bia. Vinakula sukari iliyopo katika nafaka, matunda au maziwa na kuvipa vyakula hivi tabia na ladha za pekee.[4]

Vidubini vinavyoishi ndani ya viumbehai vingine[hariri | hariri chanzo]

Vidubini vingi vinapatikana ndani ya viumbehai vingine na kupata nishati yao kutokana na lishe ya viumbehai hivi au kutokana na miili yao.

Hasa vidubini ndani ya utumbo vinasaidia kumega vyakula na kutoa virutubisho kwa ajili ya miili yetu.[5]

Vingine ni pathojeni vinavyosababisha magonjwa ya kuambukiza kwa sababu vinaongezeka ndani ya mwili na kupita kutoka mtu mmoja kwa mtu mwingine. Kuoza kwa meno kunasababishwa na bakteria zinazokula sukari mdomoni na kutoa asidi inayoharibu gamba la jino.

Inawezekana kujikinga kwa kutunza chakula vizuri, kusafisha meno na mikono na kuepukana kuwa karibu sana wa wagonjwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Rybicki E.P. 1990. The classification of organisms at the edge of life, or problems with virus systematics. S African J Sci 86: 182–6.
  2. Lwoff A. 1957. The concept of virus. J. Gen. Microbiol. 17 (2): 239–53. PMID 13481308 .
  3. Forterre P. 2010. Defining life: the virus viewpoint. Orig Life Evol Biosph. 40(2):151-60. [1]
  4. Dinorah Pous (2003). Blue Planet. McGrawHill. 
  5. Sears C.L. 2005. A dynamic partnership: celebrating our gut flora. Anaerobe 11 (5): 247–51. doi:10.1016/j.anaerobe.2005.05.001 . PMID 16701579 .

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]