Lambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lambo la Aswan kwenye Ziwa la Nasser katika Misri
Ukuta wa lambo

Lambo ni ukuta uliojengwa kwa kusudi la kuzuia mwendo wa maji au kubana maji katika eneo fulani. Mara nyingi malambo hujengwa kufunga njia ya maji ya mto. Lambo laweza pia kukusanya maji ya mvua kwenye njia ya mtelemko wake.

Shabaha ya kujenga lambo[hariri | hariri chanzo]

Shabaha ya kujenga lambo ni hasa kupata akiba ya maji. Maji hutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji, kama chanzo cha maji ya bomba kwa ajili ya watu au pia kwa utengenezaji wa umememaji.

Lambo hujengwa pia kwa shabaha ya kuzuia mafuriko.

Malambo hujengwa mara nyingi katika mabonde ambako milima ya pande zote mbili iko karibu na kupunguza mahitaji ya kujenga ukuta mkubwa mno.

Kuna pia malambo ya bahari ambayo yanajengwa kama hifadhi ya nyumba au mashamba dhidi ya maji ya bahari.

Shida za malambo[hariri | hariri chanzo]

Malabo yamekuwa pia na matatizo.

  • Ukuta unaathiri uwiano wa ekolojia kwa mfano lambo la Aswan linazuia matope yenye rutba kufika katika Misri
  • Umwagiliaji katika nchi za joto unaweza kuharibu ardhi ukiongeza chumvi katika ardhi kwa njia ya uvukizaji
  • Mara nyingi wenyeji asilia wamefukuzwa katika eneo la ziwa jipya bila kupewa makazi mazuri
  • Penye hatari ya tetemeko la ardhi uzani wa maji umeongeza matetemeko

Malambo makubwa ya Afrika[hariri | hariri chanzo]

Image:Karun3-dam.jpg

Picha za malambo[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lambo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.