Ziwa la Nasser

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lake Nasser
View from Abu Simbel
Ramani inayo onyesha eneo la ziwa
Aina ya ziwa Kiegezo
Mito ya kuingia Nile
Mito ya kutoka Nile
Nchi za beseni Egypt, Sudan
Urefu 550 km (340 mi)
Upana 35 km (22 mi)
Eneo la maji 5,250 km2 (2,030 sq mi)
Kina cha wastani 25.2 m (83 ft)
Kina kikubwa 180 m (590 ft)
Mjao 132 km3 (51,000 sq mi)[1]
Urefu wa pwani (km) 7,844 km (25,735,000 ft)
Kimo cha uwiano wa maji uso juu ya UB 183 m (600 ft)
Marejeo [1]
1 Shore urefu is not a well-defined measure.

Ziwa la Nasser (Kiarabu بحيرة ناصر buhairat nāssir) ni bwawa kubwa kwenye mto Nile iliyopatikana tangu kufungwa kwa mwendo wa Nile kwa lambo la Aswan nchini Misri kuanzia mwaka 1958.

Ziwa Nasser liko katika eneo la nchi za Misri na Sudan, hasa kati ya miji ya Aswan (Misri) na Wadi Halfa (Sudan). Eneo lake ni zaidi ya 5,200 km² lina urefu wa kilomita 550 km na upana hadi 35 km. Mjao hufikia hadi 160 km³.

Jina lilitolewa kwa heshima ya aliyekuwa rais wa Misri Gamal Abdel Nasser aliyefanya azimio la kujenga bwawa.

Faida na matatizo ya ziwa[hariri | hariri chanzo]

Kuzuiliwa kwa mwendo wa mto ulimaliza mafuriko ya kila mwaka ya Nile nchini Misri. Kwan upande mwingine matope yenye rutba hayafiki tena chini ya Aswan na wakulima wahitaji kununua mbolea wa chumvi waliporidhika zamani na matope yaliyobaki mashambani baada ya mafuriko. Vilevile matope haya yameanza kujaza nafasi ya ziwa na mjao wake umeendelea kupungua polepole.

Pia delta ya Nile katika Mediteranea haikukua tena lakini imeanza kupungukiwa.

References[hariri | hariri chanzo]