Aswan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jiji la Aswan
Mto Nile mjini Aswan
Mto Nile mjini Aswan
Jiji la Aswan is located in Misri
<div style="position: absolute; z-index: 2; top: Expression error: Unexpected < operator.%; left: Expression error: Unexpected < operator.%; height: 0; width: 0; margin: 0; padding: 0;">
Jiji la Aswan
Jiji la Aswan
Mahali pa mji wa Aswan katika Misri
Anwani ya kijiografia: 24°05′N 32°56′E / 24.083°N 32.933°E / 24.083; 32.933
Nchi Misri
Mkoa Aswan
Idadi ya wakazi
 - 275,000
Tovuti: www.aswan.gov.eg
Misikiti kuu ya Aswan
Kanisa la Kikopti la Aswan


Aswan (أسوان, Aswān pia Assuan au Assouan) ni mji wa kusini kabisa nchini Misri mwenye wakazi 200,000. Ni makao makuu ya mkoa wa Aswan. Imejulikana duniani kutokana na lambo la Aswan ambalo ni ukuta mkubwa unaozuia mwendo wa mto Nile na kusababisha kutokea kwa bwawa la Nasser.

Tangu kutengenezwa kwa lambo Aswan imekuwa mji wa viwanda kwa sababu umeme unapatikana kwa wingi tangu 1960.

Utalii ni muhimu pia kwa sababu karibu na Aswan kuna mabaki mengi ya mahekalu na majengo mengine ya enzi za Misri ya Kale.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Zamani mji ulijulikana kwa jina la Syene au Swan au Seveneh. Inatajwa katika Biblia. Ilikuwa mji muhimu wa Misri ya kusini na mara nyingi mpaka na madola ya Sudan. Hivyo Mafarao waliweka hapa kituo muhimi cha kijeshi kwa karne nyingi.

Aswan ilikuwa muhimu katika historia ya sayansi. Wazee walitambua ya kwamba wakati wa mchana jua iko juu kabisa angani na fimbo halina kivuli katika saa ya mchana. Mtaalamu Mmisri Eratosthenes alianza hapa upimaji wake uliothebitisha ya kuwa dunia si tambarare lakini duara kama mpira.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Aswan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.