Nenda kwa yaliyomo

Ziwa la Nasser

Majiranukta: 22°25′N 31°45′E / 22.417°N 31.750°E / 22.417; 31.750
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bwawa la Nasser)
mtazamo wa paneli wa ziwa nasser
Lake Nasser
Ramani inayoonyesha eneo la ziwa
Anwani ya kijiografia 22°25′N 31°45′E / 22.417°N 31.750°E / 22.417; 31.750
Aina ya ziwa Kiegezo
Mito ya kuingia Nile
Mito ya kutoka Nile
Nchi za beseni Egypt, Sudan
Urefu km 550 (mi 340)
Upana km 35 (mi 22)
Eneo la maji km2 5 250 (sq mi 2 030)
Kina cha wastani m 25.2 (ft 83)
Kina kikubwa m 180 (ft 590)
Mjao km3 132 ([convert: unit mismatch])[1]
Urefu wa pwani (km) km 7 844 (ft 25 735 000)
Kimo cha uso wa maji juu ya UB m 183 (ft 600)
Marejeo [1]
1 Shore urefu is not a well-defined measure.

Ziwa la Nasser (kwa Kiarabu بحيرة ناصر, buhairat nāssir) ni bwawa kubwa kwenye mto Nile lililopatikana tangu kufungwa kwa mwendo wa Nile kwa lambo la Aswan nchini Misri kuanzia mwaka 1958.

Ziwa Nasser liko katika eneo la nchi za Misri na Sudan, hasa kati ya miji ya Aswan (Misri) na Wadi Halfa (Sudan). Eneo lake ni zaidi ya km² 5,200, lina urefu wa kilomita 550 na upana hadi km 35. Mjao hufikia hadi km³ 160.

Jina lilitolewa kwa heshima ya aliyekuwa rais wa Misri Gamal Abdel Nasser aliyefanya azimio la kujenga bwawa.

Faida na matatizo ya ziwa

[hariri | hariri chanzo]

Kuzuiliwa kwa mwendo wa mto ulimaliza mafuriko ya kila mwaka ya Nile nchini Misri. Kwan upande mwingine matope yenye rutuba hayafiki tena chini ya Aswan na wakulima wanahitaji kununua mbolea wa chumvi waliporidhika zamani na matope yaliyobaki mashambani baada ya mafuriko. Vilevile matope hayo yameanza kujaza nafasi ya ziwa na mjao wake umeendelea kupungua polepole.

Pia delta ya Nile katika Mediteranea haikukua tena lakini imeanza kupungua.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa la Nasser kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.