Miundombinu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barabara ni sehemu muhimu ya muundombinu wa kila nchi

Miundombinu (Ing. infrastructure) ni neno la kutaja jumla la vifaa vya kiteknolojia, majengo na njia za mawasiliano inayounda muundo wa nje wa mji, dola au nchi na maisha ya wananchi wake. Vifaa vya muundombinu ni msingi wa uchumi. Kwa jumla ni vitu vya kudumu miaka mingi.

Pamoja na vifaa vya kiteknoljia kuna pia aina ya miundombinu ya kijamii unaoonekana katika upatikanaji wa elimu, huduma za afya, polisi na mahakama, pamoja na jumuiya za watu ndani ya jamii zinazotoa huduma kwa mfano makanisa, jumuiya za msikiti au mahekalu, shirika zisizo za serikali. Kwa mtazamo huo miundombinu ya kijamii ya kimsingi ni familia na ukoo.

Nchi za kisasa huwa na miundombinu ya

Kuna vingi vingine. Vifaa vya kimsingi vya miundombinu vinatumiwa na watu wengi kwa hiyo ni kazi ya umma au serikali kuvijenga na kuvitunza.

Nchi tajiri huwa na miundombinu ulioendelezwa lakini nchi maskini huwa na miundombinu kidogo tu. Mara nyingi maazimio kama kujenga barabara au kutandiza mabomba ya maji au nyaya za umeme huweka msingi kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi.