Radi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kwa maana tofauti ya neno hili kama elementi ya kikemia angalia radi (elementi)

Radi nchini Marekani
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Radi (pia: ngurumo ya umeme) ni mwangaza na miale ya mwanga wa umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Katika mazungumzo ya kila siku neno radi linaweza kutaja pia sauti yenyewe na mwanga unaweza kuitwa "umeme". Matumizi ya neno "umeme" kwa ajili ya teknolojia ya "electricity" na vifaa vya umeme yamesababisha kukaza tofauti kati ya umeme kwa jumla na kutokea kwake kwa ghafla wakati wa mvua kali kama mwangaza mkali. Hata hivyo maana ya kiasili ya "umeme" ni ule mwangaza.

Asili yake ni volteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenye chaji tofauti au pia kati ya mawingu na ardhi. Volteji hii ikiongezeka mno husababisha mkondo wa umeme hewani unaoonekana kama mwangaza mkali. Mkondo unatoa pia joto kali na joto hili husababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huu unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali lakini inawaza kusikika pia sawa na mshtuko wa mlipuko kama ni karibu.

Kama mwendo wa radi ni kutoka mawinguni kwenda ardhi unaweza kuleta hasara kwa watu au vitu. Takriban watu 2,000 hupigwa na radi kila mwaka na mara nyingi wanakufa. Radi huwasha moto kwenye nyumba au porini. Radi inayolenga ardhi huelekea kuingia sehemu ya juu mahali inapopiga. Hapa kuna mitambo ya kikingaradi ni chuma zilizopo juu ya dari ya nyumba na kuendelea hadi ndani ya ardhi kando la nyumba. Kama radi inapiga nyumba itachukua nyjia ya haraka ya kufika ardhini kwa hiyo itapita kwenye vyuma bila kuumiza nyumba yenyewe.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Radi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.