Shoti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Shoti Kizito
muhusika wa Siri ya Mtungi
ShotiKizito.jpg
Taswira ya Shoti (uhusika umechezwa na Suleiman Mambo
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Suleiman Mambo
Idadi ya sehemu 26
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kiume
Kazi yake Msaidizi wa Cheche na Gereji kwa baba yake
Familia Kizito
Ndugu Cheusi Mtungi
Dini Mwislamu
Utaifa Mtanzania

Shoti Kizito ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Suleiman Mambo. Shoti ni mtoto wa pili wa Bi. Mwanaidi na Mzee Kizito. Hajazalizwa tumbo moja na Cheusi Mtungi ambaye ni mke wa Cheche Mtungi. Kiuhalisia, Shoti ni mtoto wa Bi. Farida, lakini kutokana na kupata tabu wakati wa ujauzito wake, Bi. Farida alimkataa na hatimaye kuja kulelewa na Bi. Mwanaidi kama mtoto wake wa kumzaa. Hali hii inapelekea kuonekana Shoti kama mtoto wa Mwanaidi. Ukweli unakuja kujulikana baadaye kabisa sehemu ya 24 wakati Sabrina Kizito akihadithia mama yake wa kufikia Nusura juu ya hadithi ya Shoti. Sabrina nae alihadithiwa na mama yake Bi. Vingawaje. Shoti na Cheche ni mtu na shemeji yake. Amecheza kama hamnazo kidogo, japo anaonekana kudhibiti shughuli zake alizokabidhiwa. Mara chache sana anaingiza mkenge yale aliyotumwa. Mfano katika sehemu ambayo walikuwa wakipitia mitaani wakitangaza picha za promosheni, ukipiga picha zaidi ya moja unongeza moja bure.

Yeye alikuwa akisikika akisema kupiga picha bure kwa ajili ya promosheni maalumu. Jambo hili lilileta taharuki kubwa pale studio hasa kwa kufuatia rundo la watu waliokuja kupiga picha bure kwa gharama za Cheche. Shoti ni mtoto anayependwa sana na wazazi wake, hasa mama yake asiyependa kuona mtoto wake anapatwa na shida zozote. Hata kuna kipindi Cheche alimwacha anazagaazagaa peke yake sehemu fulani, yeye akaenda zake kwa Lulu. Huku nyuma Shoti anazishiwa zengwe lililopelekea kupigwa, lakini bahati nzuri anasaidiwa na Bonge aliyekuwa meneja wa Sharo Milionea. Bonge anachukuana na Shoti hadi baa, kanywa vya kutosha, bahati nzuri waliolewesha ndio waliomrudisha nyumbani kwao.

Jambo hili lilimhuzunisha sana mama yake Shoti, Bi. Mwanaidi, hadi kupelekea kupigwa marufu kwa Shoti kwenda kushinda studioni kwa Cheche. Ilichukua muda hadi hapo Mzee Kizito alipomruhusu Shoti arudi tena studio. Tangu hapo akawa mwangalifu sana Cheche kwa Shoti. Pamoja na kuonekana kama taahira, Shoti ni mdadisi sana wa mambo. Japo haonekani kupewa furasa ya kuyajua mambo mengi na wale wanaomzunguka. Mama yake anamlinda Shoti kupita maelezo. [1]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Shoti katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.